Habari za Punde

Wanabodi Idara ya Bandari watembelea Bandari Pemba

MKURUGENZI wa Bandari tawi la Pemba Mhe:Hamad Salim akitoa maelekezo ya bandari ya Wete, kwa wajumbe wa wakurugenzi ya shirika la bandari Zanzibar, waliofanya ziara ya siku tatu kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)



INJINIA mkuu wa shirika la bandari Zanzibar, Mbarouk Hamad akitoa maelezo ya ujenzi wa Bandari wakati walipotembelea bandari ya wete, kuangalia eneo ambalo kamapuni ya Azam Marin Inalotaka kujenga gati yake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)



WAJUMBE wa Bodi ya wakurugenzi ya shirika la bandari Zanzibar, wakikagua bandari ya wete, wakati walipofanya ziara yao ya siku tatu kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)



WAJUMBE wa Bodi ya wakurugenzi ya shirika la bandari Zanzibar, wakitoka kuangalia eneo linalodaiwa kujengwa bandari katika eneo la Mkumbuu Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)



MKURUGENZI wa shirika la bandari Zanzibar, Kepteni Abdalla Juma Abdalla, akitoa maelezo kwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la bandari Zanzibar, juu ya nyumba ya shirika hilo ambayo imekodishwa benki ya watu wa Zanzibar, tawi la Pemba huko Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)



MKURUGENZI wa shirika la bandari Zanzibar, Kepteni Abdalla Juma Abdalla, akitoa maelezo kwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la bandari Zanzibar, Juu ya hali ya bandari ya Mkoani ilivyo, huku vyombo vya usafiri vikiongezeka.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.