Habari za Punde

Dua na Uwekaji Maua Katika Kaburi la Mzee Karume

Askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania waliotayarishwa maalum kwa ajili ya kubeba mashada ya mau kwa ajili ya kuweka katika Kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Mwanamapinduzi wa Zanzibar na Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa ASP.
Rais wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif, Balozi Ali Karume na Balozi Mdogo wa China Zanzibar Balozi Tai Yanlia na kulia Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Luteni  Jenerali S.A.Ndomba.na Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Ahmeid Ameir, akiwa amekaa katika kiti.wakisubiri kuweka Mashada ya Mau katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume baada ya kusomwa kwa Dua ya kumuombea iliofanyika katika jingo la Afisi Kuu ya CCM Zanzibar. 
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwa na Mama Fatma Karume wakiwa na Wake wa Viongozi katika hafla ya kuweka Mashada ya Mau katika kaburi la marehemu Mzee Abeid Amani Karume wakati wa kumuombea Dua iliofanyika katika Jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.kulia Mke wa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Zakia Bilal na Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Shadya Karume
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka Shada la mau katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, baada ya dua ya kumuombea iliofanyika katika Jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar na kuhudhuriwa na Wananchi mbalimbali katika hitma hiyo. 
Makamu wa  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Shada la mau katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, baada ya dua ya kumuombea iliofanyika katika Jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar na kuhudhuriwa na Wananchi mbalimbali katika hitma hiyo.   
MNADHIMU Mkuu  wa JWTZ Luteni Jenerali  S.A.Ndomba  akiweka Shada la mau katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, baada ya dua ya kumuombea iliofanyika katika Jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.    
Balozi Mdogo wa China Zanzibar  Balozi Tai Yanlia, akiweka Shada la mau katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, baada ya dua ya kumuombea iliofanyika katika Jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.akiwakilisha Mabalozi Wadogo walioko Zanzibar.   
Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Ahmeid Ameir , akiweka Shada la mau katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, baada ya dua ya kumuombea iliofanyika katika Jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.ni mmoja wa Wanamapinduzi ya Zanzibar aliyeshiriki na Marehemu Mzee Karume kuikombo Zanzibar 
Mtoto wa Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Balozi Ali Karume akiweka Shada la Mau kwa niaba ya Familiya katika kaburi la Baba yao wakati wa kumuombea Dua iliofanyika katika Jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar ikiwa ni kumbukumbu ya kumkumbuka Jamadari wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Karume.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Saleh Omar Kabi akisoma dua katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, ikiwa ni dua maalum ya kumkumbuka Mzee Karume 
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwa  na Mama Fatma Karume,Bi Yasmin Aloo na kushoto Mke wa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Zakia Bilal, Mke wa Rais Mstaaf wa Zanzibar Mama Shadya Karume na Bi Asha Abdallah wakiitikia dua wakiwa katika kaburi la Mzee Karume.
Viongozi wa Serekali wakiwa katika eneo la kaburi la Mzee Karume wakiitikia dua iliokuwa ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar.
Baba Askofu Mkuu wa Zanzibar wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar Askofo , Michael Hafidh, akimuombe  Marehemu Mzee Abeid Amani Karume wakati wa kumbukumbu ya marehemu kumuombea dua, iliofanyika katika jingo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Kiongozi wa Madhehebu ya Hindu Zanzibar Bangwanji Mshaba akisoma dua katika kaburi la marehemu Mzee Abeid Amani Karume wakati wa dua ya kumuombea iliofanyika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Viongozi wa Serekali wakiwa katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM kuhudhuria Dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, kutoka kulia Mhe Haroun Ali Suleiman, Mhe Bernard Membe na Mhe Mark Mwandosa wakifuatila hafla hiyo ya dua.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika Hitma ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliofanyika leo katika jingo la Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimsikiliza Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk. Amani Karume wakiwa katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, baada ya kumalizika kwa hafla ya Dua.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akizungumza na Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Shekh. Alhad Mussa na Mhe Bernard Membe wakiwa katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar baada ya kumalizika kwa hafla ya dua leo asubuhi.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiagana na Meya wa Mji wa Zanzibar Mhe Khatib Abdurahaman Khatib, baada ya kumalizika kwa hafla ya kumuiombea Dua Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Jamadari wa Mapinduzi ya Zanzibar.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akizungumza na Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Shekh. Alhad Mussa na Mhe Bernard Membe wakiwa katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar baada ya kumalizika kwa hafla ya dua leo asubuhi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiagana na Meya wa Mji wa Zanzibar Mhe Khatib Abdurahaman Khatib na Wananchi waliohudhuria hafla ya kumuiombea Dua Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Jamadari wa Mapinduzi ya Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho akifurahia jambo na Mhe Mark Mwandosa wakiwa katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar walipohudhuria hafla ya kisomo cha kumuombea dua Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.      
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoiko Mhe Nassor Mazrui, akizungumza na waandishi wa habari maendeleo yalioletwa na Mzee Karume wakati wa uhai wake
Baba Askofo Micheil Hafidh akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali  baada ya kumalikiza kwa hafla ya dua.   
       Balozi Ali Karume akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa hafla ya dua 
Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Ahmeid Ameir akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika hafla ya dua ya kumuombea Mzee Karume iliofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar .
 Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakati alipohudhuria hitma ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.


2 comments:

  1. SubhaanaAllah siku hizi hatuna mashekhe tenakwani wao wanashindwa kukemea ouvu wa aina yoyote kwa kutaka kuwaridhisha watawala.Serikali haina dini kama wasemavyo lakoni watu wa dini na dini yetu ni Al Islam sasa kitabu gani kinacho ruhusu kufanya kumbukumbu na baya zaidi kuweka mauwa.Kuombea dua kwa maiti wetu ni sawa kabisa kwani wanihitaji huko waliko lakini haya mauwa ............Kama nimekosea naomba mwenye elimu anisaidie

    ReplyDelete
  2. mwenyezi mungu amlipe kwa yale aliyoyatanguliza kwa mikono yake ameen , kila mtu atabeba zigo lake mwenyewe , visomo hivyo havifiki popote ndugu watawala na nyie vile vile mkirudi kwa mungu mtalipwa kwa yale mnayoyatanguliza hata tukisoma hitma kila siku ni bure tu , kila mtu hulipwa kwa amali zake hii kujidanganya na hitma na mashekhe wetu feki hao

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.