Habari za Punde

Kubomoka kwa tuta la kuzuia maji kusini Pemba: wananchi walivunja mawe ya tuta hilo,

Na Mwanaisha  Moh’d  Na Kijakazi Abdallah -Maelezo 

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema sababu ya kubomoka kwa tuta hilo ni kupanda kwa kina cha maji kinachotokana na athari za mabadiliko ya tabia ya Nchi na baadhi ya  Wananachi walivunja mawe yaliyokuweko kwenye tuta hilo.

Hayo yameelezwa huko Baraza la Wawakilishi Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabibu Fereji wakati alipokuwa akijibu suala  la Mh. Saleh Nassor Juma (Jimbo la Wawi).

Alisema kuwa tuta hilo lipo Mkoa wa Kusini Pemba  Kijiji cha Jombwe na Sipwese Wananchi waliweza kulitumia tuta hilo ni kama njia ya kwenda Muambe pia wanafunzi walilitumia kwa ajili ya kwendea Skuli hiyo  mnamo mwaka 2010 tuta hilo lilianza kubomoka na kurahisisha njia ya maji ya chumvi  kupita na kuelekea  Kijiji  cha Sipwese hadi Chuo cha Mafunzo Kengeja.

Alifahamisha kuwa tuta hilo zaidi ya urefu wa mita 100  mbali ya kuwani kizuizi cha maji ya chumvi yanayoingia katika maeneo hayo  kwani  tuta hilo limetumika zaidi kama kivuko katika maeneo hayo.


Aidha alisema uingiaji wa maji ulianza mwaka 2002 wakati tuta hilo lilijengwa mwaka 2004  kutokana na kutumiwa vibaya halikuweza kuchukuwa muda mrecu likabomoka.

 Hata hivyo Serikali kwa sasa haijasaidia kujenga tuta hilo bali Mpango huo ndio utakao toa dira ya kushughulikia maeneo yalioingia maji ya chumvi ambayo yapo (145) Uguja na Pemba.

Sambamba na hayo Waziri huyo amesema juhudi za kupunguza maji ya chumvi kuelekea maeneo hayo Serikali ikishirikiana na wananchi kupitia Ushirika wa (Green Peace and Enveronmetal Conservation- GPEC) imeweza kupanda miti ikiwemo Mikoko,Mikandaa yenye urefu wa heka tatu za miti hiyo zimepandwa eneo hilo na imeweza kuendelea kustawi vizuuri kuhifadhi mazingira .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.