Habari za Punde

Walimu wa ushauri nasaha wa wilaya ya Mkoani waandalliwa semina

 AFISA Mdhamni wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Salim Kitwana Sururu, akizungumza na waalimu wa ushauri nasaha wa wilaya ya Mkoani, wakati akifungua mafunzo ya siku mbili, ya kutambulisha wasaidizi wa sheria na haki za binadamu, kulia ni Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba,
Khalfan Amour Mohamed, akifuatiwa na Mratibu wa wake, Fatma Khamis Hemed na kushoto ni mratibu wa mafunzo hayo Safia Saleh Sultan, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
  WAKILI wa serikali kutoka afisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Pemba Ali Haidar, akitoa mada juu ya chimbuko, historia ya haki za binadamu kwenye mafunzo ya siku mbili, kwa waalimu wa ushauri nasaha wa wilaya ya Mkoani, yaliofanyika Kituo cha Huduma za Sheria mjini Chake chake, ambao ndio waandaji wa mafunzo hayo, (Picha na Haji
Nassor, Pemba).
 AFISA elimu na mafunzo ya amali wilaya ya Mkoani Pemba, Seif Mohamed Seif, akichangia mada ya dhana ya wasaidizi wa sheria, iliowasilishwa na Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, kwenye mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi na haki za binadamu, kwa waalimu wa ushauri nasaha wa wilaya ya Mkoani, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MTOA mada ya ufafanuzi wa sheria ya watu wenye ulemavu, Mohamed Hassan Ali,  kwenye mafunzo ya waalimu wa ushauri nasaha wa wilaya ya juu ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria na haki za binadamu, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba, yaliofanyika mjini Chake chake, (Picha na Haji Nassor,Pemba).


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.