STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 7.7.2015
WANANACHI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wameeleza
kuwa amani, utulivu na mshikamano ndio misingi pekee ya kuleta maendeleo
endelevu hapa Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa
Kaskazini Unguja Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa aliyasema hayo, wakati akitoa
shukurani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein huko katika viwanja vya Ikulu ndogo Mkokotoni.
Aidha, Mama
Mwanamwema Shein naye aliungana na akina mama wenzake wa Mkoa huo katika futari
hiyo ya pamoja iliyoandaliwa na Alhaj Dk. Shein kwa ajili ya wananchi wa Mkoa
huo.
Katika maelezo
yake Mhe. Tindwa alisisitiza azma ya Dk. Shein ya kuendeleza amani, utulivu na
mshikamano miongoni mwa Wazanzibari na kumpongeza juhudi anazozichukua kwa
niaba ya wananchi wa Mkoa huo.
Mhe. Tindwa
alieleza kuwa amani ndio tunu ya taifa, hivyo kuna kila sababu ya kuilinda,
kuidumisha na kuitetea kwa hali zote huku akisisitiza kwa yeyote atakaejaribu
kuvunja amani aripotiwe kwenye vyombo vinavyohusika.
Alisisitiza kuwa
Waislamu wote ni ndugu hivyo kuna kila sababu ya wananchi wa Zanzibar kuendelea
kuishi kwa amani, maelewano na mapenzi makubwa miongoni mwao ili kumpwekeshwa
MwenyeziMungu.
Nae Maalim Khamis
Hassan kutoka Mkoa huo, akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wafutarishwa alisisitiza
haja ya kuendeleza ushirikiano baina ya wananchi wote.
Maalim Khamis
alitumia fursa hiyo kutoa neno la shukurani kwa niaba ya wazee wa mkoa huo kwa
futari hiyo huku wakimuombea dua Alhaj Dk. Shein azidi kuendelea kuiongoza
Zanzibar kwa amani, utulivu, mshikamano na maelewano makubwa.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail:
rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment