Habari za Punde

Bodi ya Mikopo yaongeza muda wa kuwasilisha maombi



Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo Bw George Nyatega

Na Mwandishi Wetu

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa waombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwasilisha maombi yao hadi mwishoni mwa mwezi huu (31 Julai, 2015).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumatano, Julai 15, 2015) na Mkurugenzi Mtendaji wa (HESLB) Bw. George Nyatega, hatua hiyo imechukuliwa ili
kuwapa fursa wombaji ambao hawajakamilisha kufanya hivyo.

“Hatua hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kufanya maombi ya mikopo katika  muda uliopangwa,” amesema Bw. Nyatega katika taarifa yake iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari.

Itakumbukwa kuwa awali Bodi ilianza kupokea maombi kwa njia ya mtandao (www.olas.heslb.go.tz) tarehe 4 Mei, 2015 na mwisho wa kuwasilisha maombi ulipangwa kuwa tarehe 30 Juni, 2015.

Kupitia taarifa yake, HESLB imewataka waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao hawajakamilisha maombi yao kukamilisha na kuwasilisha maombi yao ya mikopo ndani ya muda ulioongezwa na kusisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 31 Julai, 2015.

HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu.

Mwisho.

-- 

Omega S. Ngole,
Manager - Information, Education and Communication,
Higher Education Students' Loans Board,
Plot No. 8/46, Sam Nujoma Road, Mwenge Area,
PO Box 76068,
Dar es Salaam,
Facebook:www.facebook.com/people/Omega-Ngole
Twitter: https://twitter.com/OmegaNgole

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.