Habari za Punde

Changamkia ajira Unguja na Pemba

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa kada mbali mbali katika Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati - Pemba kama ifuatavyo:-

1. MWENDESHA MASHINE YA KUZALISHA KOKOTO ‘Nafasi (1)’ PEMBA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya cheti katika fani ya Mechanics kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. FUNDI KARO ‘Nafasi’ (1) - PEMBA 
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na elimu ya Cheti katika fani ya ‘Plumbing’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. 

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 30 Julai, 2015 wakati wa saa za kazi.
• Muombaji anatakiwa aiainishe nafasi ya kazi anayoiomba kati ya zilizotajwa hapo juu vinginevyo maombi yake hayatazingatiwa. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Chake Chake Pemba.



 1. WALINZI ‘Nafasi (8)’ – UNGUJA na ‘Nafasi (10)’ - PEMBA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na elimu ya Kidato cha nne (Form IV)
• Awe tayari kufanya kazi za ulinzi muda wowote.

2. ICT ‘Nafasi’ (1) 
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘ICT’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. MUHUDUMU KWA WANAFUNZI ‘Nafasi’ (1) - UNGUJA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na elimu ya Sekondari.
• Awe tayari kuishi kwa muda wote Chuoni hapo.

4. WAHUDUMU SHAMBANI ‘Nafasi’ (10) - PEMBA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari
• Awe tayari kufanyakazi za kilimo mashambani.

5. BWANA NA BIBI SHAMBA ‘Nafasi’ (10) - PEMBA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari
• Awe amemaliza mafunzo ya kilimo katika ngazi ya Cheti au Diploma kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. AFISA MSAIDIZI MISITU ‘Nafasi’ (2) - PEMBA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari
• Awe amemaliza mafunzo ya misitu katika ngazi ya Cheti au Diploma kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

7. DEREVA WA GARI ‘Nafasi’ (1) - PEMBA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari
• Awe na leseni ya udereva katika kiwango cha Class ‘B’
• Awe amepata mafunzo ya udereva katika chuo kilicjosajiliwa

8. DEREVA WA TREKTA ‘Nafasi’ (2) - PEMBA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari
• Awe na leseni ya udereva katika kiwango cha Class ‘E’
• Awe amepata mafunzo ya udereva katika chuo kilicjosajiliwa

9. FUNDI TREKTA ‘Nafasi’ (1) - PEMBA
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari
• Awe na elimu ya Cheti au Diploma katika fani ya Ufundi wa Mechanics au Automotive kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. 

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 30 Julai, 2015 wakati wa saa za kazi.
Muombaji anatakiwa aiainishe nafasi ya kazi anayoiomba kati ya zilizotajwa hapo juu vinginevyo maombi yake hayatazingatiwa. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Chake Chake Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.