Na Maryam Kidiko-Maelezo
Jumuiya ya kuhifadhisha Qur'aan ya akina Mama iliyopo Mtoni Wilaya ya Magharibi imeandaa mashindano ya kuhifadhisha qur-an kwa akina Mama watu wazima .
Mashindano hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Maruhubi yaliyojumuisha kinamama kutoka sehemu mbalimbali katika Wilaya ya Magharibi.
Mwalimu Mkuu, Ustadh Khamis Masoud Omar, kutoka Jumuiya ya Marqaz amesema lengo kuu la Jumuiya hiyo kuwashajiisha kinamama kuijua Dini yao ya kiislamu ili waweze kuisoma na kuielewa vizuri.
Amesema kuwa Jumuiya hiyo haibaguwi mtu yeyote hivyo wanapokea Waislam wanawake na watoto pia watafanya mpango wa kuanzisha kuhifadhisha Qur'aan waislam wa Kiume wakiwemo watu wazima ili kila muislam aweze kuhifadhi kitabu hicho.
Hata hivyo amesema ipo haja ya kuanzisha kuhifadhisha Qur'aan kwa wanaume watu wazima na kuwapa hamasa waislamu wengine kuanzisha mfumo kama huo ili waislamu waijue vizuri Dini yao.
Nae mshika fedha wa Jumuiya hiyo, Ukhti Latifa amesema elimu haina mwisho hivyo kila muislamu anatakiwa kuisoma na kuihifadhi Qur'aan tukufu Kitabu cha Mwenyezi Mungu .
Akitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili Jumuiya hiyo ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kusomea pamoja na uchakavu wa banda la kusomea .
Sambamba na hayo wameomba wale wenye uwezo wa kuwasaidia wajitokeze kwani wanahitaji Uzio katika Banda lao ili kuepusha vitendo vya uhalifu na kuweza kupata stara.
Jumla ya vyuo 6 vimeshiriki katika mashindano hayo yaliyojumuisha Juzuu moja hadi juzuu ya 20.
No comments:
Post a Comment