Habari za Punde

Mchezo wa Bonaza Masauni Cup Kati ya Miembeni na Mkunazini Timu Hizo zimetoka sare 1-1

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ndg Daudi Khamis Juma akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Miembeni kabla ya mchezo wao kuaza wa Bonaza wa Kombe la Masauni,uliofanyika uwanja wa mnazi mmoja usiku jana. katika mchezo huo timu hiyo imetoka sare ya bao 1--1 na timu ya Mkunazini.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ndg Daudi Khamis Juma akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Mkunazini kabla ya mchezo wao kuaza wa Bonanza wa Kombe la Masauni,uliofanyika uwanja wa mnazi mmoja usiku jana. katika mchezo huo timu hiyo imetoka sare ya bao 1--1 na timu ya Miembeni  
Kikosi cha Timu ya Miembeni kilichoilazimisha sare timu ya Mkunazini katika mchezo wa Bonaza kuwania Kombe la Masauni linalofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar Michuano hiyo kwa ajili ya kuinua vipaji vya Wachezaji Zanzibar.
Kikosi cha Timu ya Mkunazini kilichoilazimisha sare timu ya Miembeni katika mchezo wa Bonaza kuwania Kombe la Masauni linalofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar Michuano hiyo kwa ajili ya kuinua vipaji vya Wachezaji Zanzibar.
Benchi la ufundi la timu ya Mkunazini wakifuatilia mchezo wao na timu ya Miembeni mchezo uliofanyika viwanja vya mnazi mmoja timu hizo zimetoka sare ya bao.1--1. 
Mchezaji wa timu ya miembeni akimpita mchezaji wa timu ya mkunazini katika mchezo wa Bonaza wa Kombe la Masauni.
Kipa wa timu ya mkunazini Abui akiokoa mpira golini kwake wakati wa mchezo wao wa Bonaza Kombe la Masauni inayofanyika viwanja vya mnazi mmoja usiku.
Wachezaji wa timu ya miembeni na mkunazini wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Bonaza la Masauni Cup uliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja usiku.
        Mchezaji wa timu ya miembeni akiruka kihuzi cha mchezaji wa timu ya mkunazini akiwa chini.
Kipa wa timu ya mkunazini akidaka mpira huku mchezaji wa timu ya miembeni akijiandaa kuleta madhara 
Kocha wa timu ya miembeni akitowa mawaidha kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko ya mchezo huo wa Bonaza uliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar
Wachezaji wa timu ya mkunazini wakipata maelekezo kutoka kwa kocha wao wakiwa mapumziko ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo kuwania Bonaza la Masauni Cup.
Mchezaji wa timu ya mkunazini akimpita mchezaji wa timu ya miembeni wakati wa mchezo wao wa Bonaza la Masauni Cup. timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1
Wachezaji wa timu ya Mkunazini na Miembeni wakipongezana baada ya mchezo wao kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1--1, mchezo uliofanyika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar Bonaza hilo limedhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Eng Hamad Masauni 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ndg Daud Khamis Juma, akimkabidhi fedha kiongozi wa timu ya Miembeni shilingi 50.000/= zilizotolewa na Mwenyekiti wa Umija wa Wazazi Tanzania Mhe Abdalla Bulembo. kwa timu itakayoshinda mchezo huo.kukabidhiwa shilingi laki moja. 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ndg Daud Khamis Juma, akimkabidhi fedha kiongozi wa timu ya Mkunazini shilingi 50.000/= zilizotolewa na Mwenyekiti wa Umija wa Wazazi Tanzania Mhe Abdalla Bulembo. kwa timu itakayoshinda mchezo huo.kukabidhiwa shilingi laki moja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.