NAIBU
Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii , Vijana , Wanawake na
Watoto, Nd. Msham Juma Khamis akimkabidhi msaada , Pili Ahmada wakati wa
makabidhiano ya msaada wa vyakula uliotolewa na Kampuni ya simu ya Zantel.
Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel, bw Mohammed Mussa akizungumza machache kabla ya makabidhiano ya msaada wa vyakula uliotolewea na Zantel kwa ajili ya Wazee
Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazee Zanzibar
(JUWAZA), Mwadini Kutenga akiwakaribisha wageni wakati wa shughuli ya
makabidhino ya msaada wa chakula kutoka kwa Zantel kwenda kwa jumuiya ya wazee
Zanzibar
Sehemu
ya wazee waliokabidhiwa msaada wa vyakula na Zantel.
Zanzibar, 15 July 2012: Kampuni ya simu za
mikononi ya Zantel leo imetoa msaada wa vyakula kwa ajili ya mwezi wa Ramadhani
kwa makundi maalumu ya wazee hapa visiwani Zanzibar.
Msaada huo unajumuisha sukari, unga wa ngano
pamoja na mchele umetolewa katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo.
Kampuni ya Zantel upande wa Zanzibar imeainisha wazee
zaidi ya 120 wenye uhitaji wa vyakula kwenye mwezi huu wa Ramadhani walio chini
ya jumuiya ya wazee hapa Zanzibar.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kwa wazee,
Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel-Zanzibar, bwana Mohammed Mussa, amesema ni
kawaida kwa kampuni ya Zantel kusaidia makundi mbalimbali ya kijamii katika
kipindi hiki cha Ramadhani.
'Tuna furaha sana leo kuweza kusaidia jamii hii ya
wazee ambao mara nyingi wamekuwa wanasahaulika, kwani tunaamini wazee ni sehemu
muhimu sana ya jamii ndio maana Zantel leo tumeamua kutoa msaada huu ambao
unatutofautisha sana na makampuni mengine katika vipaumbele vyetu' alisema
Mussa.
Mussa aliongeza kuwa kama kampuni ya simu inayoongoza
Zanzibar, Zantel mara zote imekuwa mfano katika shughuli zake za kijamii na vipaumbele
vyake kiujumla.
Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, mgeni rasmi ndugu
Msham Abdallah, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii
Zanzibar, alisema anaipongeza Zantel kwa kushirikiana na serikali kuyasaidia
makundi ya wazee.
‘Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali katika
kulisaidia kundi hili la wazee, kwahiyo ni furaha kwetu leo kuona Zantel
imekuwa ya kwanza kusaidia kundi hili leo’ alisema bwana Abdallah.
Akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya Zantel, naibu
mwenyekiti wa jumuiya ya wazee Zanzibar, Bwana Mwadini Kutenga, alisema anawashukuru
Zantel kwa msaada huo, akisema umekuja kwa wakati mufaka hasa ukizingatia kuwa
wanakaribia kuadhimisha sikukuu ya Idi.
Hii kampuni bado inatumia jina la Zantel ? Kwani si imeshauzwa hii kwa kampuni ya Tigo ? Naona hata siyafaham haya makampuni ......mwenye uledi nayo anijulishe
ReplyDelete