Habari za Punde

Zoezi la Mikutano ya Kampeni Jimbo la Jangombe Yatia Fora kwa Wagombea

Mwenyekiti wa Mkutano wa Kampeni Jimbo la Jasngombe Ndg Jaffar Almas akitowa maelezo ya mkutano huo kabla ya kuaza kuijieleza Wagombea kwa Wananchi wa Tawi la Kwahani 

Wagombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani udiwani wakimsikiliza Mwenyekiti wa mkutano huo Jaffar Alamas akitowa maelezo kwa wagombea muda wa kujieleza ni dakika tanmo kila mgombea 

Wagombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani udiwani wakimsikiliza Mwenyekiti wa mkutano huo Jaffar Alamas akitowa maelezo kwa wagombea muda wa kujieleza ni dakika tanmo kila mgombea 
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Jangombe Ndg Abdalla Diwani akitowa sera zake kwa Wananchi wa Tawi la CCM Kwahani wakati wa mkutano wao wa ufunguzi wa kampeni uliofanyika tawini hapo na kutoa ahadi kwa Vijana Wanawake na Wazee kulipatia maendeleo Jimbo la Jangombe na kutowa fursa za Ajira kwa Vijana kupitia kazi za Amali.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Jangombe miaka ya 2010 Ndg Mohammed Rajab Soud akigombea nafasi ya Uwakilishi katika Jimbo la Jangombe baada ya kukaa nje kwa muda wa miaka mitano.  baada ya nafasi yake ya Ubunge kuchukuliwa na Mhe Hussein Mussa Mzee anamaliza muda wake sasa.
Wananchi wa Jimbo la Jangombe wakifuatilia mkutanio huo wa kampini uliofanyika katika viwanja vya Tawi la CCM Kwahani Unguja.
Mwananchi wa Tawi la CCM Kwahani akimuuliza mgombea Uwakilishi Ndg Mohammed Rajab Soud, wakati wa mkutano huo.
Ndg Ramadhan Hamza Chande akijieleza kwa Wananchi wa Jimbo la Jangombe wakati wa mkutano wao wa kwanza wa kampeni uliofanyika katika Tawi la CCM Kwahani jana.Na kkuahidi kulipatia maendeleo jimbo hilo katika sekta ya Elimu na maendeleo ili kuliinua jimbo hilo kiuchumi na kuondora kero zote ziliopo katika jimbo hilo
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Jangombe Ndg Shehe Othman Khamis, akitowa sera zake kwa Wananchi wa Jimbo la Jangombe wakati wa mkutano wa kampeni kuomba ridhaa za Wananchi kumpitisha kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu. 
Mgombea Uwakilishi katika Jimbio la Jangombe Ndg Idrisa Hussein Mrisho akitowa sera zake kwa Wananchi wa Tawi la CCM Kwahani akiowa katika kampeni ya kuwania nafasi ya kuteuliwa kugombea Jimbo hilo.
Viongozi wa kusimamia kampeni ya Jimbo la Jangombe wakifuatilia mkutano huo wakati wa Wagombea kujieleza kwa Wananchi kuhakukisha hawakiuki taratibu za Uchaguzi na kampeni.
Mgombea Uwakilishi ambaye ni Mwandisdhi wa Habari wa Kituo cha Television cha Star Tv ZAnzibar Mwarab Mmadi Mwarab akijinadi kwa kumwa sera zake kwa Wananchi wa Tawi la CCM Kwahani na Wananchi wa Jimbo la Jangombe wakati wa mkutano wa Kampeni uliofanyika tawini hapo na kutoa Ahadi kwa Vijana kuondoa kero zote katika Jimbo hilo na tatizo ya Maji.
          Ndg Mwaranb Mmad akisisityiza jambo wakati akijieleza kwa Wananchi wa Tawi hilo.
Mgombea wa Jimbo la Jangombe Ndg Mwarab Mmadi Mwarab akipongezwa na wagombea wezake baada ya kumaliza kujieleza na kuomba kura kwa Wananchi wa Tawi la CCM Kwahani,

Wagombea Ubunge Jimbo la Jangombe wakiwa mbele ya Wananchi wa Tawi la CCM Kwahani wakisubiri kutowa Sera zao kwa Wananchi hao
Mbunge wa Jimbo la Jangombe Mhe Hussein Mussa Mzee anayetetea nafasi yake hiyo akijieleza kwa Wananchi wa Tawi la CCM Kwahani kuomba riadhaa za Wananchu kurudi tena kumalizia ahadi zake katika jimbo hilo ambazo badi hazijakamilika 
Wananchi wa Jimbo la Jangombe wakifuatilia mkutanio huo wa kampini uliofanyika katika viwanja vya Tawi la CCM Kwahani Unguja.
Mgombea Ubunge Jimbo la Jangombe Ndg Mgeni Mwalimu Ali akiomba kura kwea WanaCCM wa Tawi la Kwahani na kutoa sera zake kufanikisha jimbo hilo katika maendeleo na kuahidi kama atapata ridhaa za wananchi atachukua Vijana kupata ajira katika serikali ya Muungano ya ya Zanzibar. na kutowa fursa kwa vijana kujiendeleza kielimu. katika vyuo vya Amali.
Mgombea Ubunge Jimbo la Jangombe Ndg Talib Ali Talib akimwaga sera zake kwa Wananchi wa Tawi la CCM Kwahani. 
Mgombea Ubunge Jimbo la Jangombe Ndg Abdalla Hussein Kombo akitowa sera zake na kuweka kipaumbele mambo matatu katika kulipatia maendeleo jimbo hilo kwa Wananchi wake mambo hayo amesema elimu afya na maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo ili kuweza kuwapatia kipato 
Mgombea Ubunge kwa mara ya pili katika Jimbo hilo la Jangombe Ndg Ali Hassan King akitowa sra zake kwa wananchi wa Tawi la CCM Kwahani wa Jimbo la Jangombe kuomba ridhaa zao ili kuweza kuwawakilisha vizuri na kuwapatia maendeleo katika jimbo lao hilo 
Ndg Haji Lila Haji akitowa nasaha zake kuopmba kura kwa wananchi wa tawi la CCM Kwahani wakati wa kujinadi kwa Wananchi kupata ridhaa za kukiwakilisha Chama katika Uchaguzi Mkuu mwezi wa Oktoba 2015
Waheshimiwa wagombea Ndg Mohammed Rajab na Abdalla Diwani wakifuatilia mkutano huo wa kampeni wakati wagombea wezao wakijieleza kwa wananchi katika tawi la CCM Kwahani. 
Wananchi wa Jimbo la Jangombe wakifuatilia mkutanio huo wa kampini uliofanyika katika viwanja vya Tawi la CCM Kwahani Unguja.wazee wakiwa makini kufuatilia sera za Wagombea tawini hapo 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.