Habari za Punde

Mzee wa miaka 60 alazwa Hospitali ya Wete, anahitaji kutambuliwa

Na Masanja Mabula –Pemba  .
 MTU mmoja anayekisiwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 60 amelazwa katika hospitali ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba  akipatiwa matibabu baada ya kufikishwa na wasamiria wema akiwa hali mbaya na hana fahamu .
Kwa mujibu wa Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Wete Haroub Selemani ni kuwa mtu huyo ameshindwa kufahamika jina lake na sehemu anayotoka kwani wameshindwa kupata mawasiliano na mzee huyo kwa kuwa hasemi .
Amesema kuwa kwa sasa mtu huyo anaendelea kupewa huduma muhimu  na Idara ya  Ustawi wa Jamii Wilaya ikiwa ni pamoja na matibabu ya dawa akiwa  chini ya usimamizi wa madaktari wa hospitali hiyo
Ameeleza kuwa taarifa kwa kufikishwa mtu huyo katika hospitali hiyo alipatiwa na wafanyakazi wa hospitali hiyo ili wasaidiane kumpatia huduma za matibabu pamoja na masuala mengine ya chakula  baada ya kutelekezwa na waliomfikisha hospitalini hapo .
“Nakiri kupokea taarifa za kuwepo na mgonjwa katika hospitali ya Wete akiwa hafahamiki jina lake pamoja na sehemu anayoishi , lakini kwa sasa tunaendelea kumpa matibabu tukishirikiana na madaktari wa hospitali hiyo ”alifahamisha .
Aidha Afisa Ustawi wa Jamii amesema kuwa Idara ya Ustawi Wilaya , Jeshi na Polisi pamoja na watendaji wa hospitali wanashirikiana kufanya uchunguzi ili kutambua jina la mtu huyo na sehemu anayosihi .
Katika hatua nyingine Haroub amewataka wananchi kufika hospitali ya Wete kwa ajili ya kufanya utambuzi wa mtu huyo na kisha kushirikiana na taasisi ambazo zinaendelea kumpta huduma mtu huyo .
“Nitoe wito kwa wananchi kufika hospitali ya Wete kumwangalia mtu huyo ili waweze kushirikiana na taasisi zinazotoa huduma kwa mtu huyo ambaye hali yake sio nzuri ”alieleza .
Aidha daktari ya zamu katika wodi ya wanaume hospitali ya Wete  ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwa vile sio msemaji wa Hospitali hiyo amesema kuwa bado wanaendelea kumpa huduma ya matibabu lakini hali yake sio nzuri .
Amesema kuwa tangu alipofikishwa katika hospitali hiyo hali yake sio nzuri ya kuridhisha na tayari amepewa huduma ya kwanza ikiwa  ni pamoja na kumuongezea maji .
“Tunaendelea kumpa huduma za matibabu ambapo tayari tumpatia huduma ya kwanza ya kumuongeza maji na hali yake sio mzuri kwani hawezi hata  kuongea ”alifahamisha .

Mwandishi wa habari hizi alifika ndani ya wodi ya wanaume hospitali hiyo na kumshughudia mtu huyo akiwa hana fahamu huku hali yake ikiwa tete ambapo baadhi ya wananchi wameitaka taasisi zinazohusika kuwachukulia hatua wanafamilia wa mtu huyo akiwa watajitokeza 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.