Habari za Punde

DK.Shein Akutana na Balozi Mpya wa Urusi Nchini.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na mgeni wake  Balozi wa mpya wa Urusi Mhe,Yuri F.Popov katika Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania baada ya kujitambulisha leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana  na mgeni wake  Balozi wa mpya wa Urusi Mhe,Yuri F.Popov katika Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania baada ya mazungumzo yao alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amekutana na Balozi mpya wa Urusi nchini Tanzania Mheshimiwa Yuri Popov na kumweleza balozi huyo kuwa Tanzania inathamini sana uhusiano na ushirikiano wake na nchi hiyo na kwamba kuna kila sababu za nchi mbili hizo kuundeleza na kuuimarisha uhusiano huo.

Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa wananchi wa Zanzibar wanakumbuka na kuthamini mchango wa nchi hiyo katika kipindi kipya cha ujenzi wa Zanzibar mara baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964.

“Tunakumbuka hadi leo ushirikiano wetu na iliyokuwa Shirikisho la Nchi za Kisoshalisti la Usovieti tulivyoshirikiana nao katika kujenga Zanzibar mpya” Dk. Shein alimueleza Balozi Popov.

Alibainisha kuwa katika kipindi chote hadi leo pamoja na mabadiliko yaliyotokea Tanzania na Urusi zimekuwa na uhusiano na ushirikiano wa karibu na daima nchi hizo zimeonesha dhamira za kuimarisha na kuundeleza uhusiano huo.

Kwa hivyo alikubaliana na rai ya Balozi Popov kuwa sekta ya utalii ni moja ya eneo ambalo Zanzibar na Russia zinaweza kushirikiana kwa kuzingatia kuwa Urusi ni moja ya nchi zenye kutoa watalii wengi duniani lakini wengi wahafiki katika nchi za Afrika ikiwemo Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alisema angependa kuona kasi ya ushirikiano kati ya Zanzibar na Urusi katika maeneo ya taaluma na mafunzo inaongezeka kwa kuwepo na fursa zaidi za masomo kwa vijana wa Zanzibar.

Kwa upande wake Balozi huyo wa Urusi alimueleza Mheshimiwa Rais kuwa amefurahi kupata fursa ya kuitumikia nchi yake nchini Tanzania kwa kuwa ni rafiki na ndugu wa muda mrefu wa nchi yake.

“Nimefurahi kuja Tanzania na jukumu langu la kwanza ni kuhakikisha uhusiano na ushirikiano wetu unaimarika wakati wote nitakapokuwa nchini” alieleza Balazi Yuri Popov.

Alisema katika kipindi hiki atakachokuwa nchini moja ya mambo atakayoyatekeleza ni kuhakikisha watalii kutoka nchini kwake wanatembelea Tanzania na Zanzibar ikiwemo.

Balozi Popov alifafanua kuwa hilo ni eneo ambalo linaweza kukuza zaidi ushirkiano kati ya wananchi wa nchi yake Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 
  E-mail: saidameir@ikuluzanzibar.go.tz

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.