Habari za Punde

Karatasi za kura zasambazwa katika Ofisi za Tume za Wilaya Unguja na Pemba

DSC03974
Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Uchaguzi Ya Zanzibar Ndg. Salum Kassim Ali akiwa pamoja na Afisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania akitowa maelekezo juu ya utaratibu wa usambazaji wa karatasi za kura kutoka katika Ghala kuu la Tume kwenda Afisi za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Kazi hiyo ya Usambazaji wa Karatasi za kura ilifanyika tarehe 23/10/2015 kwa ajili ya matayarisho ya upigaji kura Tarehe 25/10/2015.
DSC03994
Watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, waangalizi pamoja wawakilishi wa vyama vya siasa wakiwa makini kufuatilia zoezi la usambazaji wa karatasi za kura kutoka ghala kuu la Tume kwenda Afisi za wilaya za Tume.

DSC03999
Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika kazi ya upakiaji wa karatasi za kura kwa ajili ya kuzisambaza katika Afisi za Wilaya Za Tume Ya uchaguzi ya Zanzibar,tarehe 23/10/2015. kazi hiyo ya Usambazaji wa kura limeshuhudiwa na wajumbe wa Tume, Watendaji wa Tume, waangalizi wa Uchaguzi,Jeshi la Wananchi wa Tanzania na wawakilshi wa vyama vya siasa.
Usambazaji wa karatasi za kura umefanyika ikiwa ni miongoni mwa matayarisho ya Uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika nchini tarehe 25/10/2015.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.