Naibu Katibu
Mkuu wa UWT, Salama Aboud akielezea umuhimu wa wanawake wa Tanzania, kukiunga
mkono chama cha mapinduzi, ili kuzidi kuimarisha uchumi wao, kwenye mkutano wa
kampeni uliohutubiwa na Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe: Samia Suluhu Hassan, uliofanyika skuli ya sekondari ya Fidel
Castro Chake chake Pemba.
Katibu wa
CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Khadiji Nassor Abdi, akizunguma kwenye mkutano wa
kampeni, uliohutubiwa na Mgombea mwenza wa urais, wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe: Samia Suluhu Hassan, uliofanyika skuli ya sekondari ya Fidel
Castro Chake chake Pemba.
Mgombea Mwenzawa
urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Mhe: Samia Suluhu
Hassan, akizungumza na wanawake wa chama hicho wa wilaya nne za Pemba, kwenye
mkutano uliofanyika skuli ya sekondari ya Fidel Casto wilaya ya Chake chake.
Wahamasishaji wakiongozwa Mhe: Faida Mohamed Bakari (kulia),
wakiimba wimbo maalumu kwenye mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Mgombea urais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Samia Suluhu Hassan, uliofanyika skuli
ya sekondari ya Fidel Castro Chake chake Pemba
Wanawake wa
CCM wa wilaya nne za Pemba, wakiwa na furaha kubwa, mara baada ya Mgombea
Mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwa tiketi ya chama hicho
Mhe: Samia Suluhu Hassan, alipowasili kwenye ukumbi wa skuli ya sekondari ya
Fidel Castro wilaya ya Chake chake, kumuombea kura mgombea urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe: John Pombe Magufuli
No comments:
Post a Comment