VIONGOZI wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa
kaskazini Pemba, wakiongozwa na mkuu wa Mkoa huo Mhe:Omar Khamis Othman,
wakikagua ekari 20 za msitu wa wanajamii zilizoteketea kwa moto zenye thamani
ya Milioni 200/=, huko Kikunguni Kigongoni Shumba Viamboni Wilaya ya Micheweni
Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA.)
LICHA ya wananchi na kikosi cha Zimamoto na Uwokozi
Wilaya ya Wete Kisiwani Pemba, kujitahidi kuuzima moto ulioteketeza zaidi ya
Ekari 20 za msitu wa hifadhi ya jamii zenye thamani ya shulingi Milioni 200/=,
huko Kikunguni kigongoni shumba Viambani lakini bado baadhi ya maeneo moto huo
haukukubali kuzimika.(Picha na Abdi
Suleiman, PEMBA.)
SHEHA wa Shehia ya Mihogini Shumba Viamboni Wilaya
ya Micheweni Salim Said Salim, akizungumza na waandishi wa habari mbali mbali,
juu ya athari iliyopatikana baada ya zaidi ya Ekari 20 kuteketea kwa moto za
msitu wa Hifadhi ya wanajamii wa Kikunguni Kigongoni shumba Viamboni Wilaya ya
Micheweni kisiwani pemba.(Picha na Abdi
Suleiman, PEMBA.)
KATIMU mkuu wa Wilaya ya Micheweni, ambaye pia ni
mkuu wa Wilaya ya Wete Mhe:Hassan Khatib Hassan, akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kukagua eneo la msitu lililoathirika na moto na kuteketeza
zaidi ya Ekari 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 200/=, huko Kikunguni
Kigongoni Shumba Viamboni Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKUU wa Mkoa wa kaskazini Pemba Mhe: Omar Khamis
Othman, akitoa tamko la Serikali ya Mkoa wake na kuwapa pole wananchi waliopata
hasara ya kuunguliwa msitu wao wa wanajamii na kuteketeza zaidi ya ekari 20
zenye thamani ya Milioni 200, huko Kikunguni Kigongoni Shumba Viamboni Wilaya
ya Micheweni Kisiwani Pemba.(Picha na
Abdi Suleiman, PEMBA.)
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba Mhe:
Hassan Nassir Ali, akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamko la Jeshi la
polisi, dhidi ya watu waliofanya hujma za kuichoma moto msitu wa wanajamii na
kutekeketeza zaidi ya Ekari 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 200, huko
kikunguni Kigongoni Shumba Viamboni Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
No comments:
Post a Comment