Habari za Punde

Nyumba ya naibu Sheha , Tibirinzi yachomwa moto na watu wasiojulikana




NYUMBA ya Naibu sheha wa shehia ya Tibirinzi wilaya ya Chake chake Pemba, Bikombo Simai Juma (42), ambayo imedaiwa kuchomwa moto na watu wasiofahamika kwa madai ya hitilafu za kisiasa, tukio hilo lilitokea oktoba 26, majira ya saa 7:00 usiku, ambapo wakati huo alikuwa ndani amelala na jumla ya watu 13 akiwemo mtoto mchanga wa mwezi mmoja, walisalimika kufa, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

: NYUMBA nyengine ilioko kando mwa nyumba ya naibu sheha, eneo hilo la Tibirinzi, kijiji cha Minazini, ikiwa imechomwa moto nyuma kwenye eneo la choo cha makuti, inayomilikiwa na Khamis Kassim Juma siku hiyo hiyo ya Oktoba 26 usiku wa saa 7:00 ambapo matukio yote hayo hakuna aliejeruhiwa, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
NAIBU sheha wa shehia ya Tibirinzi wilaya ya Chake chake Pemba Bikombo Simai Juma (24) akizungumza na mwandishi wa habari hizi hayupo pichani, muda mfupi baada ya nyumba yake kudai kutiliwa moto na watu wasiofahamika, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.