Habari za Punde

Uzinduzi wa Maktaba ya Umoja wa Mataifa kwa Vijana wa Jumuiya ya Umoja wa Mataifa Zanzibar.

Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar.

Wazanzibar wametakiwa kujifunza zaidi kuhusu kazi za umoja  wa Mataifa Nchini na Duniani kote kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao.

Hayo yameelezwa leo huko Kinazini Unguja katika Jengo la Shirika la Biashara (ZSTC) na Alvaro Rodriguez wakati wa ufunguzi wa Maktaba ya Umoja wa Mataifa  na Ofisi ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana Zanzibar.

Amesema ni vyema Wazanzibari kujitokeza kwa wingi katika  Maktaba ili kujifunza masomo mbali mbali  kwani fursa pekee itakayowawezesha kukuza elimu yao.

Mratibu Mkaazi huyo emeeleza kuwa kituo cha Maktaba hiyo kitatoa machapisho na Vijarida vya Umoja wa Mataifa na vifaa vyengine mbali mbali ambavyo vinaweza kutumika kusaidia Vijana na watu wazima kuongeza ufahamu wao wa kazi za Shirika ikiwa ni njia ya kuendelea tamaduni ya usomaji.

Aidha amesema Ofisi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa Tanzania (YUNA) ya Unguja na Pemba zitakuwepo katika Maktaba hiyo pia itafanya kazi ya kuongeza ufahamu wa kazi za umoja kati ya vijana na pia kuhamasisha vijana kushiriki katika harakati za kuleta maendeleo.

Hata hivyo Tanzania inavyoanza safari yake ya kufikia malengo ya maendeleo endelevuifikapo 2030,maktaba ya Umoja wa Mataifa na (YUNA) itasaidia sana katika kufikisha malengo ya Dunianikwa watuna hasa kwa Vijana wa Zanzibar.

(YUNA) inaundwa navikundi 43 vya umoja wa Mataifa Mashuleni na kati ya hivyo vikundi sita viko Zanzibar vikiwa na wanachama wapatao 1,355.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.