Habari za Punde

Waziri SMT aangushwa jimboni Pemba


Na waandishi Wetu, Pemba
MATOKEO  ya ubunge, uwakilishi na udiwani yameanza kutangaazwa na maofisa wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo kadhaa kisiwani Pemba, baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji wa kura hapo juzi.
Kazi ya kuhesabu kura za urais, ubunge na uwakilishi karibu majimbo yote   ya Pemba, ilimalizika kati ya saa 5:00 usiku na baadhi ya majimbo, kama ya Mkoani na Mtambwe  kumalizika kwa zoezi hilo kwa siku ya pili.
UBUNGE
Jimbo la Chambani wilaya ya Mkoani kwa tiketi ya CUF mgombea wake Yussuf Salim Hussein ameibuka na ushindi baada ya kupata kura 4,966, na kumshinda mpinzani wake aliegombea wa chama cha mapinduzi CCM Mohamed Abrhaman Mwinyi, aliepata kura 749, chama cha CHAUSTA, kura 35, ADC kura 63 wakati chama cha ACT kwa nafasi ya ubunge imejikusanyia kura 23.
Jimbo la Ole wilaya ya Chake chake, lililokuwa na wagombea watano, CUF iliibuka na ushindi baada ya mgombea wake Juma Hamad Omar kujizolea kura 4464, huku mpinzani kwa Omar Mjaka Ali wa CCM alikipata kura 753, ADC kura 44, NRA 50, na chama cha CHAUSTA kimepata kura 42 kilichokuwa na mgombea mwanamke pekee Tatu Abdalla Msellem. 
Kwa upande wa Jimbo la Mtambile, Chama cha wananchi CUF kimetetea kiti chake kwa kupata kura 5106, huku chama cha Mapinduzi CCM kikijikusanyia kura 878, wakati ADC kikijikusanyia kura 95 mbele ya ACT kilichopata kura 195.
Jimbo la Kiwani wilaya ya mkoani, CCM kupitia mgombea wake Rashid Abdalla Rashid alijipatia kura 1772, wakati CUF kupitia mgombea wake Abdalla Haj, ndie ilieibuka na ushindi kwa kupata kura 3,731, huku chama cha ADC kikijipatia kura 95, huku ACT kikipata kura 25.
Jimbo jengine ambalo mgombea wa CUF Tahiri Awesu aliibuka mshindi ni jimbo la Mkoani, kwa kujizolea kura 6,734, mgombea wa CCM Pro: Makame Mnyaa Mbarawa, yeye alijipatia kura 3,656, vyama vyengine kwenye kura zao kwenye mabano, TADEA kura (24), ACT (15), DP (31), NRA (21) na chama cha UPD kilipata kura (11) za ubunge.

Jimbo la Micheweni CUF kupitia mgombea wake Haji Khatib Kai aliibuka na ushindi kwa kupata kura 4,279, CCM kupitia mgombea wake Khamis Juma Omar alipata kura 1,406, Shoka Khamis Juma aliekuwa mbunge wa CUF mwaka 201O kabla ya kufukuzwa na kuhamia ADC, alipata kura 83, huku chama cha CHAUSTA Zena Ali Mwadini aliepata kura 42, sawa na TADEA kura kama hizo.
Jimbo jipya la Wingwi, chama cha wananchi CUF kimeibuka na ushindi kwa mgombea wake Kombo Juma Hamad, kwa kupata kura 4,469, na kumshinda mgombea wa CCM Khamis Shaame Hamad aliepata kura 442, wakati chama wa ADC chenyewe kikipata kura 27, na chama cha ACT kikijinyakulia kura 43.
Kwa upande wa Jimbo la Tumbe chama cha wananchi CUF kimeendelea kutetea kiti chake cha ubunge, na sasa kitawakilishwa na Rashid Ali Abdalla, baada ya kujizolea kura 4,788, na kumshinda Rashid Kassim Abdalla wa CCM alieibuka na kura 486, na chama cha ADC, kikijipatia kura 37, juu ya ACT kilichopata kura 57.
Katika Jimbo la Mgogoni wilaya ya Wete, mgombea CUF dk Suleiman Ali Yusuf, ameibuka mshindi kwa kujipatia kura 5,660 na kumshinda mgombea wa CCM, Issa Juma Hamad aliepata kura 669, huku ADC (24), ACT kura (16), Jimbo la Gando mgombea wa CCM Salim Issa Bakari, kashindwa baada ya kupata kura 808, huku mgombea wa CUF, Othman Omar Haji akiibuka kidedea, kwa kupata kura 6,111, CCK kura 15, ADC 17 na ACT kura 52.
Jimbo la Wete mjini, lililokuwa na vyama vinne, mgombea wa CUF, Mbaruk Salim Ali ameibuka na ushindi kwa kupata kura 4,950, na kumshinda mgombea wa CCM, dk Adballa Salehe Abdalla aliejikuta na kura 910, chama cha ADC 28 na ACT kikijipatia kura 29.
Kwenye Jimbo la Kojani, CUF imeibuka tena na ushinda kupitia mgombea wake Hamad Salim Maalim, kwa kujinyakulia kura 7,950, wakati Massoud Ali Mohamed wa CCM akiondoka na 1,054, mgombea wa CHAUSTA Khamis Suleiman Ali (82), Bakar Hassan Hama wa AFP (66), Fatma Zubeir Ali wa ADC (28), Khamis Faki Mgau wa NRA kura 88 na Ali Makame Issa wa ACT mejipatia 128.
Jimbo la Wawi lililokuwa na wagombea 12, mgombea Mohamed Juma Ngwali wa CUF, ndie aliibuka na ushindi kwa kujizolea kura 5,532, na kumshinda Daud Ismail Juma wa CCM aliepata 1,214 na vyama vyengine kura zao kwenye mabano CHAUMMA (12), CHAUSTA (15), NRA (16), SAU (14), TLP (113), UDP (9), UPDP (7), mtoto wa aliekuwa mgombea wa urais wa Zanzibar Khairat Said Sud wa AFP amejipatia kura (97) ADC (108) na chama cha ACT kura 34.
Kwenye Jimbo la Chonga kwa nafasi hiyo ya Ubunge, CUF imeshindwa ikiwakilishwa na Mohamed Juma Khatib, kwa kupata kura 3,609, wakati CCM kiliondoka na kura 1,667 ikiongozwa na mgombea wake Abdalla Omar Muya, CHAUMMA 51, huku chama cha TLP kura 49, AFP 18, ADC 17, na ACT kimepata kura 14.
Kwa upande wa Jimbo la Chake chake ambalo lilikuwa na vyama nane, CUF kilitetea kiti chake baada ya mgombea wake Yussuf Kaiaza Makaem kuibuka na ushindi kwa kujizolea kura 4,924, CCM kura 1,145 chini ya mgombea wake Mbarka Said Rashid, UDP 47, ADC kura 44, ACT 23, JAHAZI kura 13, CHAUSAT kura 16 na TLP kimepata kura sita (6).
Jimbo la Ziwani wilaya ya Chake chake Chama cha wananchi CUF kilitetea kiti chake baada ya mgombea ubunge wa Jimbo hilo Nassor Suleiman Omar kujikusanyia kura 5,484, na kumuacha Mohamed Othman Omar wa CCM aliepata kura 609, AFP kura tisa (9), ADC 14, TLP 31, UPDP kura 13, huku      
UWAKILISHI
Jimbo la Ziwani kulikokuwa na wagombea wa vyama vinne, huku CUF ikiibuka na ushindi kwa kupata kura 5,540, CCM kura 600, ADC 30 na UPDP kura 27, wakati Jimbo Chonga CUF kimetetea kiti chake kwa kupata kura 3,836, CCM kura 1,521, ACT 29 na ADC kura 28.
Kwenye jimbo la Chake chake mjini, CUF iliondoka na ushindi kwa kujipatia kura 4,329 chini Omar Ali Shehe, Suleiman Zaharan wa CCM amepata kura, 660, ADC 28 na chama cha  ACT kura 46, huku Jimbo la Wawi mgombea wa CUF Khalifa Abdalla Ali akiibuka na ushindi kwa nafasi hiyo, baada ya kupata kura 5,275, na kumuangusha mgombea wa CCM Hamad Abdalla  Rashid Gerei aliepata kura 1,289, ADC 128, ACT kura 36, na chama cha CHAUMMA kura 24.
Jimbo la Mkoani CUF, iliibuka na ushindi kupitia mgombea wake Seif Khamis Mohamed aliepata kura 6,983, na kumshinda mpinzani wake wa CCM Mmnga Mjengo Mjawiri aliekuwa Chuo kikuu Zanzibar SUZA, aliepata kura 3,414, TADEA kura 51, ADC kura 46, na chama cha ACT kwa jimbo hilo kimepata kura 15.
Majimbo ambayo hayajapatikana matokeo yake hadi waandishi wetu wanaondoka kwenye vituo vya majumuisho ni pamoja na majimbo Konde, Mtambwe, Ole na Micheweni kwa nafasi za uwakilishi

        

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.