Habari za Punde

Mkutano wa 20 wa Kimataifa wa Wanasheria wa Afrika Mashariki Wafanyika Zanzibar katika Hoteli ya Sea Cliff

Katibu wa Chama cha Wanasheria Zanzibar Mhe Omar Said Shaban akitowa maelezo kwa Washiriki wa Mkutano huo kabla ya kufunguliwa Rasmin na Jaji Mkuu wa Zanzibar. uliofanyika kastika ukumbi wa hoteli ya Sea Cliff Zanzibar.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wa Kimataifa wa 20 wa Wanasheria wa Afrika Mashariki wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano.
Rais wa Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki Mhe Nossor Khamis akizungumza wakati wa Mkutano huo wa 20 wa Wanasheria wa Afrika Mashariki uliofanyika Zanzibar katika Ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar na kumkaribisha Mgeni Rasmin Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu kwa ajili ya kuufungua mkutano huo wa Siku Mbili. 
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu akifungua Mkutano wa Kimataifa wa 20 wa Wanasheria wa Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar unaozungumzia Huduma za Wanasheria kwa Ajamii na kutoa huduma hiyo kote katika Nchi za Afrika Mashariki na nje ya Afrika. 
Washiriki wa Mkutano huo wakiwa katika ukumbi wa Mkutano wakimsikiliza mgeni rasmin akiwahutubia na kuwafungulia mkutano wao wa siku mbili kuzungumzia Huduma ya Sheria kwa Wateja wao. 

Baadhi ya Washiriki kutoka sehemu mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.
Katibu wa Chama cha Wanasheria Afrika Masharki Godfrey Nathan Kitiwa akitowa maelezo ya Mkutono huo wa 20 wa Wanasheria wa Afrika Mashariki katika ukumbi wa Sea Cliff Zanzibar.

Mtoa Mada kutoka Kenya Dr Otiende Ammollo akitowa Mada wakati wa Mkutano huo wa Kimataifa wa Wanasheria wa Afrika Mashariki uliofanyika Zanzibar katika Ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar nje kidigo ya Mji wa Zanzibar.














No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.