Habari za Punde

Naibu Katibu Mkuu , Miundombinu na mawasiliano akagua madhara ya mvua kwa barabara Pemba

 Wajumbe wa Bodi ya barabara Zanzibar wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mhe: Tahir Abdalla mwenye suti na kutia mkono mfukoni,  wakishuka gari na kukagua eneo ambalo Wizara hiyo Pemba imelifukia kwa mawe kwa ajili ya kuzuwia barabara kuliwa na maji ya mvua, karibu na kituo cha Polisi Mkoani.
Mhandisi Mkaazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Pemba Khamis Massoud, akitoa maenelezo kwa wajumbe wa bodi ya barabara kutoka wizara hiyo, wakati walipofika kukagua shimo lenye urefu wa mita 15 lililofukiwa kwa mawe karibu na kituo cha Polisi Mkoani.
 Wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Pemba, wakipanga mawe katika shimo hilo lenye urefu wa mita 15 ambalo limegharimu zaidi ya gari 200 za mawe, katibu na kituo cha polisi Mkoani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa barabara Zanzibar Mwalim Haji Ameir, akimuonesha mmoja wa mjumbe wa bodi hiyo njia ambayo maji ya mvua hupitia na kusababisha kuvubuka kwa shimo kubwa pambeni ya barabara katibu na kituo cha Polisi Mkoani.
(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.