Habari za Punde

Matukio ya Picha Mitaani Zenj

Wananchi wakiwa katika harakati za kujipatia mahitaji yao ya kila siku katika Soko Kuu la Mwanakwerekwe Zanzibar hupatikana bidhaa zote za matunda na nafaka katika Soko hilo maarufu katika Mji wa Zanzibar. 

 Ona magari yanavyopita kwa tabu eneo hilo likiwa na barabara kubwa tu ya kupita magari mawili kwa wakati mmoja
Jama Mtu kama huyu gari yake ikipigwa loki nani wa kumlaumu jamani. Bila ya kujali matumizi ya barabara hii kuu ya Michenzani hutumika kwa magari mengi yakiwemo magari ya abiria daladala, ameegesha gari lake na kuweza kuchukua nafasi kubwa ya barabara ikizingatiwa eneo hilo ni la krosi na jirani na raundi abauti ya michezani. 
Vibarua wa Kampuni inayojenga mtaro wa maji katika uwanja wa mpira wa Mnazimmoja wakiwa kazini katika ujenzi huo. Mtaro huu utasaidia kuweza kusafirisha maji ya mvua kupeleka baharini na kukifanya kiwanja hicho kuchezeka wakati wote wa kiangazi na mvua.
Mambo ya Mitandao hayo.
 Vijana wakiwa katika katika jengo la Afisi ya Zanlink wakipata huduma ya WIFI kupitia simu zao za mkononi kupata habari mbalimbali kutoka Nje na Ndani ya Zanzibar kupitia simu zao na kuwasiliana na  Afisi Ndugu na Jamaa kwa urahisi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.