Habari za Punde

Naibu Waziri wa Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Bihindi Aikabidhi Vifaa vya Michezo Timu ya Zanzibar Beach Soka Inayoshiriki Michuano ya Afrika Mashariki Nchi Kenya.

Mjumbe wa Kamati Tendaji ya ZFA Mwalim Masoud Attayi akizungumza wakati wa hafla hiyo. 
Katibu wa Baraza la Michezo Zanzibar Mwalim Khamis akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Vifaa kwa Timu ya Ufukweni ya Zanzibar Beach Soka.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar ( BMZ ) Sharifa Khamis, (Shery) akizungumzia Mchezo wa Soka la Ufukweni Zanzibar (Beach Soka) wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na Naibu Waziri wa Michezo Zanzibar katika ukumbi wa VIP Amaan Zanzibar. 
Viongozi wa Michezo Zanzibar wakihudhuria hafla ya kukabidhiwea Vifaa vya Michezo Timu ya Zanzibar Beach Soka 
Viongozi wa Zanzibar Beach Soka wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe Bihindi Hamad wakati wa hafla ya kukabidhiwa Vifaa vya Michezo vya Beach Soka katika ukumbi VIP Amaan Zanzibar.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii Michezo Zanzibar Mhe Bihindi Hamad akizungumza na Wanamichezo wa Mchezo wa Mpira wa Ufukweni Zanzibar (Beach Soka) wakati wa kuwakabidhi Vifaa vya Michezo kwa Uongozi wa Timu hiyo katika ukumbi wa VIP Amaan Zanzibar. 

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe Bihindi Hamad akimkabidhi Vifaa vya mchezo wa Soka la Ufukweni (Beach Soka ) Kiongozio wa Timu hiyo Ali Shariff (Adof) kwa ajili ya timu yake kuweza kushiriki vizuri katika michuano hiyo ya Afrika Mashariki inayofanyika Nchini Kenya makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa VIP Uwanja wa Amaan Zanzibar.katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Sharifa Khamis (Shery)
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe Bihindi Hamad akimkabidhi Vifaa vya mchezo wa Soka la Ufukweni (Beach Soka ) Kiongozio wa Timu hiyo Ali Shariff (Adof) kwa ajili ya timu yake kuweza kushiriki vizuri katika michuano hiyo ya Afrika Mashariki inayofanyika Nchini Kenya makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa VIP Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kiongozi wa Timu ya Zanzibar Beach Soka Ali Shariff Adof akitowa shukrani wakati wa kukabidhiwa Vifaa vya Michezo kwa ajili ya Kushiriki Timu yao katika Michuano ya Afrika Mashariki Yanayofanyika Nchini Kenya.
 Waandishi wa Habari wa Michezo Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya makabidhiano ya Vifaa vya Michezo kwa Timu ya Zanzibar Beach Soka inayoshiriki Michuano ya Kalbu Bingwa Afrika Mashari Nchini Kenya. makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kiongozi wa Timu ya Zanzibar Beach Soka Ali Shariff (Adof) akitowa shukrani kwa Uongozi wa Wizara ya Michezo Zanzibar kwa msaada huo na kuitaka Wizara na Baraza la Michezo Zanzibar kuitilia nguvu Michezo ya Beach Soka Zanzibar ili kuukuza mchezo huo hapo Zanzibar, Timu ya Beach Soka inashiriki Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Nchini Kenya michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika Wiki Hii Nchini Kenya 
Imetayarishwa na Othman Mapara.blogspot.
Zanzinews.com.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.