Habari za Punde

Nilichokibaini baada ya ziara ya Balozi Seif mtaa wa Mlandege na kutoa amri ya zuio la ujenzi



Nilichokiona

Hivi Karibuni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alimuagiza Mmiliki wa Kiwanja kinachotaka kujengwa Nyumba ya Ghorofa katika Mtaa wa Mlandege Bwana Anwar Abdulla kusitisha mara moja ujenzi huo kufuatia malalamiko makubwa yaliyotolewa na wakaazi wa Mtaa huo wakimshutumu Mmiliki huyo kuvamia pia eneo la wazi (Open Space ) la shughuli za kijamii katika sehemu hiyo.

Nikiwa kama mwananchi ninaefuatilia kwa karibu matukio ya nyumbani , clip hii ya video inaonesha mambo mengi ambayo kwa maoni yangu serikali yapasa kuyafanyia kazi kwa karibu ili kuleta ufanisi. hapa nitayataja machache tu niliyobaini.

1    Ziara hii sijui kama ilipangwa au ilikuwa ya ghafla kwa sababu inavyoonekana Balozi Seif hakuwa na taarifa za kutosha za kiini cha mgogoro huu,. Kilichopaswa kufanyika kwanza ilikuwa kukusanya taarifa za kutosha kwa kukutana na watendaji wa Serikali kwanza ofisini na kujinikaisha na maelezo ya serikali ili wakati wa kwenda kwenye sehemu Balozi ana Taarifa za kutosha.

2     Kutokuwa na nidhamu ya kuzungumza mbele ya kiongozi mkuu wa Serikali kwani kila mmoja alikuwa akisema bila ya kuwa na mwongozo/msimamizi wa kuchagua nani aseme na kipi kifuate.

3      Maelezo ya watendaji wa serikali na uwezo waliopewa  yanaonekana kama hayaheshimiwi na wananchi au kutokuwa na nguvu ya kisheria. Suala muhimu la kujiuliza ni kwanini yasiheshimiwe?. ikiwa wakurugenzi wane wamelisimamia suala hili na bado mwananchi ameendela kujenga katika eneo lililolalamikiwa na kuonesha jeuri kwa wakaazi, hivi Wakurugenzi wetu hawana mamlaka ya kutosha kulishughulikia suala hili hadi kumuita Makamu wa Rais? Kuna nini hapa kinachopaswa kurekebishwa?

4   Je Baraza la Manispaa lina mamlaka ya kutoa kibali cha ujenzi? Mkurugenzi wa Mipango miji anatoka kibali gani kama ilivyo kwa mkurugenzi wa mamlaka na hifadhi ya mji mkongwe? Ipo haja ya kuangaliwa tena utendaji na ukasimu wa mamlaka hizi ili kuepusha migongano isiyohitajika.

Mnaweza kubaini zaidi ya haya kama mtaipitia tena 'clip' hii na kuweza kuishauri serikali yetu kwa lile litakaoisaidia  kutekeleza wajibu wake kikamilifu.

Na Mdau 



   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.