Habari za Punde

Tamasha la Masafa Lafana Ifakara, Vijana Wengi Wajengewa Uwezo wa Kutumia Ndoto Zao..

 Baadhi ya vijana wakiwa wanaendelea kufanya usafi maeneo ya Uwanja wa Taifa wa Ifakara eneo ambapo Tamasha hilo la Msafara lilifanyika.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bw. Yahya Naniya(aliyevaa miwani) akiwa katika ushiriki wa kufanya usafi kaika uwanja wa Taifa wa Ifakara
 Mwenyekiti wa Maandalizi wa Msafara kutoka TYDC James Isdore akielezea maana ya msafara kwa wakazi wa Ifakara
  Baadhi ya wakazi wa Ifakara wakiendelea kusikiliza kinacho endelea 
Mbunge wa Kilombero Mh.Peter Lijuakali akielezea Historia ya Maisha yake na mpaka amefanikiwa kuwa Mbunge, na kuwasihi vijana wengine wasikate tamaa kwa sababu kila jambo lina wakati wake

 Baadhi ya watoto wa shule mbalimbali za Msingi katika mji  wa Ifakara wakiwa katika Tamasha la Msafa
Suhaila Thawer kutoka Oxfam akiendelea kutoa utaratibu wa tamasha hillo.
 Kikundi cha young Feminist forums wakiwa wanatoa somo kwa vijana pamoja na burudani kwa njia ya ngonjera
 Mmoja wa wadau akiwa anatoa neno la kuwajenga vijana juu ya kujitambua lakini pia kuwajengea uwezo  vijana kuwa wafumbuzi na wabunifu ili waweze pata kujitambua
 Bi. Nusura Salum akitoa ushuhuda wake wa namna alivyo anza maisha yake kwa kuuza maandazi , kuwa mkulima na sasa mfanyabiashara mkubwa na alivyopitia katika safari yake ya mafanikio
 Mwanamuziki Chipukizi wa Bongo Fleva anayeishi Morogoro One Darin akitoa Burudani wakati wa Tamasha la Msafara
 Ramadhani Lyasa akielezea kwa ufupi jinsi alivyopitia changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokusoma na kuwa alianza na kilimo na sasa ni mfanyabiashara
 MC Fadhiri akiendelea kutoa utaratibu wa wazungumzaji katika Tamasha la Msafara
 Bi. Veronica Malwata mkazi wa Ifakara akieleza jinsi alivyotaka kukata tamaa ya maisha baada ya kushindwa endelea na shule na baadae kujiinua kwa kuanza kufanya kazi katika moja ya Zahanati kama muhudumu na baadae alipelekwa shule ya uuguzi na sasa ni muuguzi katika Hospitali ya Ifakara.
 Kijana Narsis nae akitoa ushuhuda wake wa yale aliyopitia mpaka amefanikiwa kaika maisha.
 Baadhi ya waandaaji wa Msafara wakiwa wanatoa neno la Shukurani kwa wakazi wa Ifakara.
Baadhi wa wanavyuo wakiendelea kufuatilia Msafara. (Picha zote na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa Tanzania)

Vijana wengi wa Ifakara Wilayani Kilombero mkoani Morogoro wamepewa nasaha kutumia vipaji vyao kwa lengo la kutimiza ndoto zao ili maisha yao yaende sawa na kukuwa kiuchumi
Mwenyekiti wa Programu ya Msafara James Isdore akizungumza  wakati wa uzinduzi wa programu ya msafara wilayani Kilombero kata ya Ifakara alisema asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 14-15 wamekuwa wakijirudisha nyuma kutumia vipaji vyao kutimiza ndoto zao kwa sababu mbalimbali.

"Tumeamua kuja Ifakara kwa lengo la kuja kuinua vijana kupitia  programu hii ambapo programu hii kwa sasaa ipo katika majaribio inatarajia kuanza rasmi mwakani 2016 hadi sasa majaribio ya programu hii yameweza kufanyika katika mikoa miwili Dar es Salaam na Ifakara na matokeo yake tumeanza kuona ni makubwa mno katika kusaidia jamii ya vijana kutimiza ndoto zao na sio kukaa vijiweni kudidimiza ndoto zao"alisena Isdore

Alisema Programu hiyo inaendeshwa kwa kupitia mashirika matano yanayojishughulisha na masuala ya vijana yakiratibiwa na Shirika la Oxfam Tanzania.


  Veronica  Malwata ambaye ni Mkazi wa mji wa Ifakara alisema ndoto ya kipaji haiwezi kuja hivi  hivi bila kujituma hivyo vijana wanapaswa kupambanua wapi walipo na wanataka kwenda wapi.

 Ramadhani Lihapa ni mmoja wa vijana ambaye alifanikiwa kutimiza ndoto zake, alisema kijana  anapaswa kujitambua ananafasi gani katika jamii na kuona ni namna gani anaweza kufikia ndoto yake aliyekuwa anaiwaza siku nyingi.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.