Habari za Punde

ZLSC: Zijuweni Katiba za Vyama vya Wafanyakazi Kabla ya Kujiunga

Na Haji Nassor, Pemba
WAFANYAKAZI wa serikali na mashirika ya umma nchini, wametakiwa kutokumbatia vyama vya wafanyakazi kabla ya kuzisoma na kuzielewa vyema katiba za vyama hivyo, ili kujua faida watakayoipata baada ya kujiunga.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, alipokua akizungumza na waandishi wa habari afisini kwake mjini Chakechake, juu ya kuwepo kwa kundi la wanachama wa vyama hivyo, wasioelewa katiba za vyama hivyo.
Alisema hakuna uharaka wa mfanyakazi kukimbilia kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi, pasi na wakuu wa vyama hivyo kuwaomba katiba na kuisoma, ili kujiepusha na migogoro ambayo inaweza kukepukika.
Mratibu huyo alieleza kuwa, inawezekana ndani ya vyama hivyo kuna mikato mikubwa au kutowekwa wazi haki za mwanchama, sasa ikiwa mwanachama hakuchukua juhudi za kuiona katiba anaweza kupoteza haki zake hata anapokumbwa na matatizo.
Aidha alifafanua, kwa vile kwa mujibu wa sheria za kazi na ajira hakuna kulazimishwa kwa mfanyakazi kujiunga na chama chochote cha mfanyakazi, hivyo ni vyema uhiari huo ukaambatana na kufahamu malengo ya chama kabla ya kujiunga.
“Hakuna haja wala mantiki kwa mfanyakazi yeyote wa serikali au hata mashirika binafsi, kujiunga na chama asichokielewa dira, dhamira na haki zake zilizotajwa ndani ya katiba’’, alifafanukua.
Kuhusu upatikanaji wa sheria mbali mbali za ajira, za kazi au mahusiano kazini, aliwashauri wanaohitaji kukitumi Kituo cha Huduma za Sheria ambacho kinamaktaba maalum.
Alifafanua kuwa, kwenye kituo chao zipo sheria ambali mbali na iwapo kuna mfanyakazi anaehitaji masaada wa kisheria unapatikana kituoni hapo bila ya malipo.
Mwanakombo Baraka Makame mwalimu skuli ya Mtambile Mkoani,  alikiri kuwepo kwa wafanyakazi waliojiunga na vyama hivyo bila ya ridhaa zao na bila ya kufahamu katiba za vyama hivyo.
“Hata mimi mwenyewe nilijikuta natenzwa nguvu kujinga na chama cha wafanyakazi, pasi na kupewa katiba wala kuelezwa kwa undani’’, alifafanua.
Mapema Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Pemba, Khalfan Amour Mohamed, alisema suala la kuijunga na vyama vya wafankazi ni jema iwapo haki itatendeka.

Katika siku za hivi karibuni, wafanyakazi serikali na mashirika binafsi, waliowengi waliojunga na vyana vya wafanyakazi wamekuwa walitafuta njia ya kujitoa kwa madai ya kutotendewa haki. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.