Habari za Punde

Mwili wa Marehemu Asha Bakari Wawasili Zanzibar kwa Mazishi Kesho Saa nne Jangombe

Ndege ya Shirika la Ndege la Qatar ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikiwa na Mwili wa Marehemu Asha Bakari alifariki nchini Dubai akitokea matibabuni Nchini India.Mareheme anatarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya Kianga nje kidogo ya mji wa Unguja na Maiti itasaliwa katika msikiti Mkuu wa Kwamchina saa nne asubuhi. 
Mwili wa Marehemu ukiteremshwa katika ndege kwa ajili ya maandalizi ya mazishi kesho saa nne asubuhi Jangombe Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Pandu Amaer Kificho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud wakiwa uwanja wa ndege Zanzibar wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu
Ndugu na Jamaa wa Marehemu wakiwa na Viongozi wa Serikali na Chama wakisubiri kuupokea mwili wa Marehemu Uwanja wa Ndege wa Zanzibar leo jioni
Mwili wa Marehemu ukishusha katika gari baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar wakiubeba wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege Zanzibar. 
Wananchi wakiupokea mwili wa Marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Wafanyakazi wa Uwanja huo leo jioni.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho na Viongozi wengine wa Serikali na Vyama vya Siasa na Wananchi wakiuombea dua mwili wa marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili Zanzibar leo jioni tayari kwa mazishi kesho katika kijiji cha kiyanga. 

Ndugu na Jamaa wakiwa na huzuni baada ya kuupokea mwili wa marehemu leo jioni Wananchi wakishiriki katika kuombeleza msiba wa marehemu Asha Bakari Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar aliyefariki Nchini Dubain wakati akitokea Nchini India katika matibabu.
Ndugu na Jamaa na Wananchi wakishiriki katika dua ya kuuombea mwili wa Marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili nyumbani kaka wa marehemu kwa ajili ya matayarisho ya mazishi kesho katika mtaa wa jangombe  
Waombolezaji wakiwa katika msiba jangombe kwa ndugu wa marehemu wakisubiri taratibu za mazishi kesho saa nne asubuhi.
Ndugu wa marehemu wakiomboleza msiba wa ndugu yao nyumbani kwao jangombe Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud akizungumza na Ndg wa c na mareheme baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu Jangombe kwa nduga zake kwa mazishi kesho
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
Zanzinews.com

1 comment:

  1. inna lillahi waina illahim rajiun

    poleni sana wafiwa wote ndugu na jamaa.
    salaam kutoka NYC

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.