Habari za Punde

Tanzania Kukumbwa na Mafuriko ya El - Nino - Umoja wa Mataifa.

Na MwandishiMaalum, New   York

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kwamba Tanzania  

ni kati ya nchi kadhaa ambazo zinawezekano mkubwa wa kukumbwa na mafuriko ya takayo sababishwa na  El- Nino.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi anayehusika na Misaada ya  Ki-binadamu na Uratibu wa Misaada ya Dharura, Bw Stephen O’Brien, kipindi ambacho  Tanzania inaweza kukabiliwa na mafuriko ya  El-Nino ni kati ya mwezi Januari na Machi mwaka huu wa 2016.

Nchi nyingine ambazo zinawezekano wa kukumbwa na mafuriko 

makubwa pamoja na  Tanzania ni  Madagascar,   Malawi na 

Msumbiji.

Taarifa ya Bw. O’Brien kuhusu madhara ya  El-Nino na namna 

gani Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kujiandaa au inajiandaa na 

kadhia hiyo iliyowasilishwa mbele ya wajumbe wa nchi 

wanachama wa Umoja wa Mataifa na nakala yake kutumwa kwa 

Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  

pamoja na kutoa tahadhri hiyo, amewasihi nchi ambazo 

zinatarajiwa kukubwa na maafa ya  El -Nino kujiandaa ipasavyo.

Maandalizi hayo ni pamoja utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa 

wananchi watarajiwa wa athari za El- Nino .

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi, 

kwa upande wa Afrika ya Mashariki,  

nchi kadhaa hususan ukanda wa magharibi zimekumbwa na uhaba 

mkubwa wa mvua na hivyo kuathiri kiwango cha upatikanaji wa chakula.  

Nchi hizo ni Ethiopia  Sudan, Djibouti na Eritrea, ilihali baadhi ya nchi zikipata kiwango cha mvua kilichovuka mipaka.

“Kuanzia mwezi Januari hadi Machi, nchi za Tanzania,  Msumbiji, 

Madagascar na  Malawi zinauwezekano mkubwa kwa kukumbwa na mafuriko ya El- Nino”.anatahadharisha O’Brien Kwa mujibu wa Bw. Stephen O’Brien nchi hizo zitahitaji pamoja na mambo mengine misaada ya kujiandaa na kushughulikia ya kile kinachokabiliwa kwamba kinauwezekano mkubwa wa kutokea.

Ukiacha nchi za Afrika ya Mashariki,nchi nyingine kwa upande 

wa Afrika ambazo zinakumbwa na hali tete ya uhaba wa mvua 

nahivyokutishiausalamanaupatikanajiwachakulani  

Angola,   Botswana, Malawi, Namibia, AfrikayaKusini, 

Swaziland, Zambia na   Zimbabwe.

Nchi hizi zimekumbwa na uhaba mkubwa wa mvua kiasi kwamba 

na kwa mujibu wa Bw. Stephen O’Brien zitakabiliwa na uhaba 

mkubwa wa chakula ambapo watu zaidi ya milioni

28 katika mataifa hivyo watakabiliwa na uhaba wa chakula

Akizungumzia kuhusu misaada ambayo imekwisha kutolewa na 

nchi wahisani katika kukabiliana na ukame na madhara yatokanayo na El-Nino,  Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi anasema kuwa hadi wakati anatoa taarifa yake kiasi  cha dola 360 milioni kilikuwa kimetolewa na wafadhili kwa lengo la kukabiliana na madhara yatakayotokana na El-Nino ukiwamo usalama wa chakula.

Pamoja na michango hiyo,   Bw. O’Brien anasema haitoshi kutokana na ukweli kwamba maafa yatakayotokana na madhira ya El-Nino yanahitaji misaada zaidi Mbali ya nchi za kanda ya Afrika baadhi ya nchi ulimwenguni ambazo zinatakumbwa na ambazo zimeshakubwa na balaa la El-Nino ni pamoja na Nchi ambao zimo katika  Bara la Latini ya  Amerika, na nchi za eneo la Pacific ambazo nyingi ni visiwa.


Shirika  la Kimataifa la  Hali ya Hewa ( World Meteorogical 

Organization) litanatarajiwa katika mwezi    February 

kutoa taarifa zaidi kuhusu mwelekeo wa El-Nino

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.