Habari za Punde

Balozi Seif amtembelea Muasisi wa ASP na Mwana Mapinduzi, Mzee Hamid Ameir

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Muasisi ya  Chama cha Afro Shirazy Party na Mwana Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Hamid Ameir ndani ya wiki ya maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 39 ya Chama cha Mapinduzi { CCM }.
 Mzee wa Chama cha Mapinduzi Mzee Ali Hassan Khamis akisalimiana na Muasisi wa ASP na Mwana Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Hamid Ameir  alipofika kumtembelea nyumbani kwake Mtoni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Anayeshuhudia kati kati yao ni Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi.

 Muasisi wa ASP na Mwana Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Hamid Ameir kati kati akibadilishana mawazo na Balozi Seif pamoja na Mzee Ali Hassan Khamis walipofika nyumbani kwake Mtoni kuzungumzia  Maendeleo ya Chama cha Mapinduzi ndani ya miaka 39 tokea kilipoasisiwa mwaka 1977 Visiwani Zanzibar.

Mzee Hamid Ameir akisisitiza umuhimu wa kuimarishwa kwa Chama cha Mapinduzi kilichozaliwa katika mifupa ya Vyama vilivyoleta Uhuru na Mapinduzi katika ardhi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania vya TANU na ASP.

Picha na –OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.