Habari za Punde

Hatuwezi kufanya mabadiliko kwa mashinikizo- Tanzania

 Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi  Tuvako Manongi, akichangia majadiliano ya Bodi ya  Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto ( UNICEF) hapo siku ya  jummane. Katika  mchango wake, Balozi amewaeleza wakuu wa UNICEF kwamba,  mabadiliko ya kweli  yanayolenga  kuboresha  hali bora ya maisha ya  makundi yote ya jamii, wakiwamo  watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali hayawezi kufanyika kwa mashinikizo kutoka nje bali yatafanyika kwa  ushiriano na ubia wa dhati baina ya Serikali,  Wadau wa Maendeleo na  Wananchi wenyewe. Vile vile Balozi Manongi akasisitiza kwamba UNICEF inapashwa kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia bajeti iliyojipangia badala ya kutegemea  misaada kutoka kwa wahisani,   hususani Asasi zisizo za kiserikali  kwa kile alichosema,  mara nyingi  Asasi hizo hutoa misaada yao kwa  malengo ya kushinikiza ajenda zao  na maslahi binafsi,
Mkutano huo  pia ulipokea na kupitisha mpango kazi wa utekelezaji wa miradi ya UNICEF pamoja na  rasimu ya Ripoti  ya Tanzania  ambayo imeainisha  masuala  mbalimbali pamoja na miradi  ya maendeleo inayorajiwa kutekelezwa na UNICEF kwa  Tanzania. Aliyeketi  na  Balozi ni  Afisa wa  Uwakilishi  Bi.Ellen Maduhu
Meza kuu ya  Wakurugenzi na Watendaji wa UNICEF wakati wa mkutano  wa  Bodi hiyo uliofanyika siku ya jumanne na kuhudhuriwa na   wajumbe wa Bodi hawapo picha pamoja na wajumbe wengine waalikwa. Tanzania ilialikwa katika mkutano huo  kama  msikilizaji. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.