Habari za Punde

Timu ya Mabaharia Weusi Black Sailors Waweka Rekodi ya Mwaka Ligi Kuu ya Zanzibar.

Na: Abubakar Kisandu. 

Timu ya Black Sailors (Mabaharia weusi) ambayo inashiriki ligi kuu ya soka Zanzibar hadi sasa ndiyo timu pekee kutoka uraiyani ambayo inafanya vyema katika ligi hiyo wakiwa ana alama 25 wakishika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Mabaharia hao weusi wameweka historia hiyo baada
 ya kuwafunga waongozaji wa ligi hiyo klabu ya JKU bao 1-0 lililofungwa na Abdul Azizi Seif (Ngasa).

Kikosi hicho kinachofundishwa na Juma Awadh baba mzazi wa kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba Awadh Juma ndiyo timu pekee kwa msimu huu iliyowahi kuzifunga timu mbili zinazoiwakilisha 

Zanzibar kwenye mashindano ya kimataifa Mafunzo na JKU.

Mbali ya rikodi hiyo pia Sailors inarikodi nyengine ya kuwa timu pekee mpaka sasa iliyocheza michezo mitatu mfululizo bila ya kuruhusu nyavu zao kutikiswa na wapinzani.
Kama hiyo haitoshi kikosi hicho bado hakijafungwa na timu yoyote ya mitaani kama vile Miembeni,Kimbunga, Mtende Rangers, Jang’ombe Boys, Kijichi na Chuoni.

Black Sailors ilianzishwa mwaka 1981 na ni msimu
wake wa kwanza kucheza ligi kuu ya soka Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.