Habari za Punde

DK Shein: Wananchi wana matumaini makubwa na barabara zinazojengwa kuunganisha nchi zetu

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                    03 Machi, 2016

---
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi 

Dk. Ali Mohamed Shein leo alikuwa miongoni mwa viongozi 

wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki 

walioshuhudia uwekaji wa jiwe la msingi la barabara ya 

Arusha- Holili kwenda Taveta hadi Voi nchini Kenya.

Akitoa salamu zake kwa viongozi na wananchi 

waliohudhuria hafla hiyo Dk. Shein alisema ujenzi wa 

barabara hiyo ni hatua muhimu ya kuzidi kuimarisha 

ushirikiano kati ya wananchi wa Tanzania na Kenya pamoja 

na nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika 

Mashariki.

“Wananchi wa Tanzania na Kenya ni watu wamoja wenye 

historia moja na utamaduni unaofanana hivyo ujenzi wa 

barabara hii utazidi kuwaunganisha na kuzidisha ushirikiano 

wetu katika nchi wanachama” Dk. Shein alisema.

Dk. Shein aliongeza kuwa wananchi wa Tanzania na Kenya 

wamejenga matumaini makubwa kwa ujenzi wa barabara 

hiyo ambao alieleza itarahisisha usafiri wa barabara kati nchi 

mbili hizo na kuinua biashara.

Aliwaeleza maelefu ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo 

ambayo ilihudhuriwa na viongozi wa nchi wanachama wa 

jumuiya hiyo kuwa Zanzibar iko pamoja na jumuiya katika 

kutekeleza miradi mikubwa kama huo ambayo umelenga 

kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi wa nchi 

wanachama.

Katika hafla hiyo iliyofanyika huko Tengeru Wilaya ya 

Arumeru Mkoa Arusha Dk. Shein alimshukuru Rais wa 

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe 

Magufuli kwa kumualika kuhudhuria mkutano wa 17 wa 

kawaida wa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya 

Afrika Mashariki pamoja na hafla hiyo ya kushuhudia utiaji 

jiwe la msingi la barabara hiyo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi 

alikuwa miongoni mwa viongozi waliohudhuria mkutano wa 

17 wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika 

katika hoteli ya Ngurdoto mkoani Arusha.

Katika mkutano huo Tanzania iliombwa na kukubali 

kuendelea kuwa mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa mwaka 

mwingine 2016/2017 baada ya kumaliza kipindi cha mwaka 

2015/2016 ambapo ilikuwa mwenyekiti.

Aidha mkutano huo ulipitisha azimio la kukubali ombi la nchi 

ya Sudan Kusini kuwa mwanachama wa Jumuiya hiyo na 

kufanya jumuiya hiyo sasa kuwa na nchi wanachama 6.

Mkutano huo ulimteua pia Rais wa zamani wa Tanzania 

Mheshimiwa Benjamin Mkapa kuongoza timu ya usuluhishi 

ya mgogoro wa Burundi ambapo Rais Museveni atakuwa 

ndie Msuluhishi Mkuu wa mgogoro huo. Mkutano huo 

uliagiza mgogoro huo upatiwe ufumbuzi wa harara 

iwezekanavyo.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla ya uwekaji wa 

jiwe la msingi leo ni pamoja mwenyeji wao Rais John Pombe 

Magufuli, Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Rais Uhuru 

Kenyatta wa Kenya.


Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.