Habari za Punde

Makocha wa Yanga wakiperuzi!

BAADA ya saa za kazi, nao waalimu wa klabu ya Yanga, ambayo ipo kisiwani Pemba Kocha Mkuu Plum na Kocha Msaidizi. Juma Mwambusi, hupata muda wa kuperuzi mitandao mbali mbali, wakati walipokuwa uwanja wa Gomani Chakechake Pemba, ambapo kikosi kilipiga kambi kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara baina yake na Azam unaorajiwa kupigwa Jumamosi ya tarehe 9 mwezi huu, 

Mwambusi alisema wachezaji wengi wote wanaendelea vizuri na mazoezi chini yao, na kuwa wamejipanga kuhakikisha kikosi chao kinashinda katika mchezo huo.
Yanga inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu, baada ya kufikisha pointi 46, sawa na Azam, lakini wanapishana kwa tofauti ya magoli, imeweka kambi visiwani Pemba, kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Azam FC.
(Picha na Haji Nassor, Pemba) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.