Habari za Punde

Ligi Daraja la Kwanza Taifa Sita Bora Kuwania Kupanda Daraja la Kwanza, Kati ya Timu ya Chwaka Star na Strong Fire Timu Hizo Zimetoka Sare ya Bao 1--1

 Mgeni Rasmin wa Mchezo wa Ufunguzi wa Ligi ya Daraja la Kwanza Taifa, Sita Bora kuwania kupanda Daraja Mbunge Mteule wa Jimbo la Kijitoupele Zanzibar Mhe Shamsi Vuai Nahodha akifuatilia mchezo huo kati ya Strong Fire ya Unguja Kuu na Chwaka Star ya Chwaka mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1, kushoto Rais wa ZFA Ndg Ravia Idarus Makamu Mwenyekiti wa BMZ Ndg Khamis 
Wapenzi wa Mchezo wa Soka Zanzibar wakifuatilia mchezo huo wac Ligi ya Sita Bora Daraja la Kwanza Taifa mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan.

Kocha Mkuu wa Timu ya Chwaka Stars Salum Mohammed Ubaya, akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo wao na Timu ya Strong Fire ya Unguja Ukuu, na kueleza mchezo uliokuwa mzuri ila wachezaji wake wameshindwa kuzitumia nafasi walizopata katika dakika za mwisho wa mchezo huo nav kutoka sare ya bao 1-1 ikiwa ni mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Sita Bota Daraja la Kwanza Taifa mchezo uliofanyika uwanja wa Amaann Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.