Naibu Katibu Mkuu wa Habari, Utalii Michezo na Utamaduni, ndugu Issa Mlingoti amefungua mafunzo ya miezi 6 ya ufugaji nyuki huko Makunduchi.
Katika nasaha zake amewata wananchi wa Makunduchi kuhifadhi misitu ili kuwalinda nyuki. Aidha amewata washiriki wa mafunzo hayo kujitahidi kwenye masomo yao na kuitumia taaluma watakayoipata kwa vitendo.
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na bibi Christin Strömberg kutoka Sweden chini ya mashirikiano kati ya wadi za Makunduchi na Manispaliti ya Sundsvall.
No comments:
Post a Comment