Habari za Punde

Vyama visivyo na uwakilishi Bungeni vyathibisha kushiriki uchaguzi Mkuu wa marudio wa Zanzibar.

Umoja wa  vyama visivyo na uwakilishi bungeni vimethibisha  kushiriki uchaguzi Mkuu wa marudio wa Zanzibar utakaofanyika Jumapili ijayo ya  Machi 20.
Vyama hivyo ni pamoja na DP, CCK, SAU, AFP, TLP, ADA TADEA, UPDP, D. MAKINI, NRA, UMD, CHAUSTA NA ADC.
Uthibitisho huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa chama cha Democraty Party (DP) Abdul Mluya kwa niaba ya mwenyekiti wa makatibu wakuu wa umoja huo.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema wamefikia hatua hiyo kutokana na vyama vyao  kuitambua tume ya uchaguzi ya zanzibar (ZEC) ndio chombo pekee chenye mamlaka ya kutangaza tarehe ya uchaguzi kwa mujibu ya sheria na katiba ya Zanzibar ya 1984.
kwa kuwa  vyama hivi vilishiriki uchaguzi wa rais Oct 25, 2015 vikiwa na imani na Tume ya Uchaguzi  kwa imani hiyo ndio maana vyama hivi vilishiriki uchaguzi huo wa awali, hivyo hatunabudi kushiriki uchaguzi wa marejeo ili demokrasia ishike mkondo wake na mshindi apatikane”. amesema Abdul MluyaAmewaomba wananchi wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kuamua hatma yao kwa miaka mitano ijayo na kuliomba jeshi la polisi kusimamia amani pamoja na uchaguzi ili uwe wa amani.

Nae katibu mkuu wa umoja huo Rovatus Muabhi amewataka mabalozi, taasisi na mashirika ya kimataifa kuacha kuingilia masuala ya siasa nchini kwa vile Zanzibar ni nchi na matatizo yaliyopo yatatatuliwa na wazanzibari wenyewe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.