Habari za Punde

Waatalam wa Takwimu Wakubaliana Mfumo wa Viashiria vya Agenda 2030

Na MwandishiMaalum, New York

Wajumbe wa Kamisheni yaTakwimu ya Umoja wa Mataifa,( UNSC) wamekubaliana juu ya mfumo ambao utatumika kupima 

utekelezaji wa Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ( Agenda 

2030) Makubaliano hayo yamefikiwa mwishoni mwa wiki wakati 

wajumbe  24 wanaounda Kamisheni yaTakwimu ya Umoja wa 

Mataifa,  pamoja na wadau wengine walipokutana kwa mkutano 

wao wa 47 uliodumu kwa wiki moja.


MkurugenziMkuuwaOfisiyaTaifayaTakwimu, Dr. Albina Chuwa aliongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  

katika mkutano huu, ambapo Tanzania ilishiriki kama Mjumbe wa Kundi la Waatalamu kuhusu Viashiria vya Mendeleo Endelevu (Inter-Agency Expert onIndicators  of Sustainable  Development Goals).

Pamoja na kujadiliana kuhusu viashiria na umuhimu wake 

katika kupima utekelezaji wa Agenda-2030,washiriki wa mkutano huu pia walijadili ajenda nyingine zilizohusu takwimu za wakimbizi,program ya ulinganifu wa kimataifa wa  data,na misaada ya kitakwimu katika utekelezaji wa Agenda  2030.

Agenda  2030  inamalengo 17 yakiwa pia na viambatisho 169 na ilipitishwa rasmi naViongozi Wakuu wa Nchi na Serikali mwezi Septemba mwaka jana na utekelezaji wake umeanza mwezi Januari mwaka huu.

Ajenda imebeba maudhui ya “kubadili dunia yetu: ajenda ya mwaka 2030 kwa maendeleo endelevu”. 

Ni ya kihistoria ikijumuisha masuala yote muhimu yanayowahusu na kugusa maisha ya kila mtu na ikiwakilisha matarajio makubwa ya maendeleo ya dunia nzima.

Inaelezwa  pia kwamba ni ajenda ya watu, ambayo imesheheni mipango ya kutokomeza umaskini wa aina zote, bila kumwacha mtu yeyote nyuma. Ikilenga pia kuhakikisha Amani na usalama, kuongeza ufanisi katika shughuli za maendeleo na kubuni ubia unaojali binadamu na sayari Duniani.




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.