Habari za Punde

Dk Shein kuongoza kikao cha kamati maalum ya NEC kesho

TAARIFA RASMI KUHUSIANA NA
KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA NEC ZANZIBAR
 KWA VYOMBO VYA HABARI.

KAMATI Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanziba, kesho (Aprili 23, 2016) inatarajia kukutana chini ya Mwenyekiti wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Itikadi na Uenezi Mama Waride Bakari Jabu imesema kikao hicho kitafanyika Afisi Kuu ya CCM, iliyopo mtaa wa Kisiwandui, Mjini Unguja.

Taarifa imesema kikao hicho kawaida cha siku moja, pamoja na mambo mengine kitapokea na kujadili taarifa kadhaa kutoka Idara na Vitengo mbali mbali vya Chama hicho, ikiwemo taarifa ya hali ya kisiasa ya Zanzibar, kabla na baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Marudio wa Zanzibar.

Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, kilichofanyika  April 20, mwaka huu, chini ya M/kiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai, kwa ajili ya kuandaa ajenda za kikao hicho.

Taarifa  imesema kikao hicho kinafanyika kwa mujibu wa Ibara ya 114 (b) ya Katiba ya CCM, Toleo la mwaka 2012 na kwamba maandalizi yote yamekamilika.
Mwisho.
Sgd.
(Waride B. Jabu),
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,
Idara ya Itikadi na Uenezi - CCM,
ZANZIBAR.
22/04/2016.

1 comment:

  1. Jamani uchaguzi tumemaliza na hali ya zanzibar ni shwari kwanini hatumpi Dr. nafasi ya kufanya kazi?

    Mimi naamini chama kina viongozi mahiri ktk ngazi zote na hawashindwi kujadili hali ya kisiasa ya zanzibar kabla na baada ya uchaguzi na hatimae kumkabidhi ripoti Dr. shein.

    Na sisi tunahitaji kufuata kasi ya wenzetu tanzania bara angalau robo kama sio nusu! chama chetu kinatawala pande zote kwani sisi tubaki nyuma wakati sera ni zile zile?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.