Habari za Punde

Balozi Seif Aongoza Mkutano wa Wawakilishi wa CCM Kumchagua Mnadhimu wa Baraza Afisi Kuu Kisiwandui Zanzibar.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasili katika ukumbi wa mkutano wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM Zanzibar kumchagua Mnadhimu wa Baraza wa CCM.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM wakiwa wamesimama wakati akiingia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi, aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo wa kumchagua Mnadhimu wa CCM katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akifungua mkutano wa kumchagua Mnadhimu wa CCM katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kuwachagua Wajumbe Watano wa NEC kupitia Wawakilishi wa CCM, mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi wakati akiufungua mkutano huo katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Wazee wa CCM Zanzibar wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akifungua mkutano huo. 
Wazee wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa uchaguzi wa Mnadhimu wa Baraza. 
Mwenyekiti wa Wazee wa CCM Zanzibar Mzee Khatib Ramadhani akizungumza wakati wa mkutano huo wa kumchagua Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi wa CCM.

Wazee wa CCM wakimsikiliza Katibu wa Wazee wa CCM Zanzibar akisoma risala wakati wa Mkutano huo uliofanyika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.