Habari za Punde

Mbio za Mwenge Wilaya ya Mjini Unguja ya Zindua Mradi wa Barabara Jimbo la Mpendae Zanzibar.

Kikundi cha Beni kikitowa burudani wakati wa uzinduzi wa barabara ya Jimbo la Mpendae Zanzibar iliojengwa kwa Fedha za Mfuko wa Jimbo na kuzinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa  wakati wa mbio za Mwenge katika Wilaya ya Mjini Unguja.
Barabara ya ndani katika Jimbo la Mpendae ikisubiri kuzinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Mwananchi wa Jimbo la Mpendae Zanzibar akisoma risala ya Wananchi wa Jimbo hilo kwa Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru wakati wa mbio zake katika Jimbo la Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg Goerge Jackson na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Mhe Mohamnmed Mahmoud, wakisikiliza risala ya Wananchi wa Jimbo la Mpendae wakati wa Hafla ya uzinduzi wa barabara ya Jimbo hilo iliojengwa kwa mfuko wa jimbo. 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg Goerge Jackson akiondoa kipazia kuashiria kuizindua Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Jimbo la Mpendae Zanzibar wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Mjini Unguja. 
Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar Mhe Salim Turky ,Mkuu wa Wilaya ya Mjini na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wakishangilia baada ya uzinduzi wa barabara hiyo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg Goerge Jackson, akikata utepe kuashiria kuzindua rasmin barabara ya Jimbo la Mpendae Zanzibar iliojengwa kwa Mfuko wa Jimbo kushoto Mbunge wa Jimbo la Mpendae Mhe. Salim Turky na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe Mohammed Dimwa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg Goerge Jackson na Viongozi wa Jimbo hilo na wananchi wakishangilia baada ya kukata utepe wa uzinduzi wa barabara hiyo.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg Goerge Jackson akimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo. 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg Goerge Jackson akimpongeza Mwakilishi wa Jimbo hilo. 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru akitembea katika barabara hiyo baada ya kuizindua barabara hiyo akiwa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo 
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.