Habari za Punde

Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Makumbusho Duniani May18.

Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid  Ali Juma akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonyesho ya kudumu ya sanaa katika  maadhimisho ya Makumbusho Duniani yaliyofanyika Makumbusho ya  Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Divisheni ya Makumbusho Zanzibar Khamis Abdalla akimuonyesha Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo sanaa ya ufumaji kofia za asili ya Zanzibar katika maonyesho ya sanaa yanayofanyika makumbusho ya Mnazimmoja.
Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma akiangalia kazi ya ubunifu iliyofanywa na msanii Naaman Ali Khamis wa kwanza (kulia) anaetumia majani makavu ya migomba. 
Mkuu wa Divisheni ya Makumbusho kutoka Idara ya Mkumbusho na Mambo ya Kale, Khamis Abdalla akisoma risala ya wafanyakazi wa Idara hiyo katika ufunguzi wa maonyesho ya sanaa  ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Makumbisho Duniani yaliyofanyika Makumbusho ya Mnazimmoja Zanzibar.
Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma akizungumza na wafanyakazi na wananchi walioshiriki maonyesho ya sanaa katika maadhimisho ya ya siku ya Makumbusho Duniani yaliyofanyika Makumbusho ya Mnazimmoja Zanzibar.
Baadhi ya viongozi wa Wizara na wageni waalikwa waliohudhuria ufunguzi wa maonyesho ya sanaa katika maadhimisho ya siku ya Makumbusho  Duniani yaliyofanyika  Mnazimmoja Mjini Zanzibar wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi.
(Picha na Makame Mshenga/Maelezo)

Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Habari, Utalili, Utamaduni na Michezo Zanzibar Rashid Ali Juma amewataka  wananchi wa Zanzibar kutumia fursa ya  kutembelea Jengo la Makumbusho  ya Mnazimmoja ili kuelewa historia ya  utamaduni  wao .

Waziri Rashid ameyasema hayo katika Sherehe za ufunguzi wa maonesho ya kudumu ya sanaa katika maadhimisho ya  siku ya makumbusho dunuani yaliyofanyika  Makumbusho ya Mnazi mmoja  Mjini Zanzibar.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  itaendelea kutoa misaada katika Idara ya Mkumbusho na Mambo ya kale ili isibakie nyuma katika ulimwengu  wa sasa  ambapo dunia imekuwa kama kijiji.

Waziri  wa Habari, Utalii Utamaduni na Michezo  amesema wananchi wanahitaji kutunza kumbukumbu na niwajibu kuyatunza maeneo  hayo yasipoteze haiba yake ya asili.

Katibu Mkuu  wa Wizara ya Habari, Utalili, Utamaduni na Michezo Zanzibar Omar Hassan Omar  amesema jengo la makumbusho ni muhimu na linapaswa kutuzwa  kwani mila, desturi na silka za Zanzibar  zinapotea  kutokana na  kukosekana  uhifadhi mzuri.

Aidha ameahidi  kushirikiana na wafanyakazi  wa Idara  hiyo kwa  kuwapatia mafunzo  ya mara kwa mara ili wawe na uwezo wa kutekeleza kazi  zao  kwa ufanisi zaidi .

Katika Risala yao iliyosomwa na Mkuu wa Divisheni ya Makumbusho Khamis Abdallah,  wafanyakazi hao wamesema  wameamua kuandaa maonyesho hayo ya kudumu ya sanaa ili kutoa mwamko na hamasa kwa jamii juu ya upana wa sanaa hiyo.

Wamesema wanajukumu kubwa la kulinda, kuhifadhi  na kutunza  kumbukumbu za taifa  lakini wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la maeneo ya kihistoria kuvamiwa na  wananchi.

“Tunajikuta tunajukumu kubwa kwa Serikali na hata kwa mwenyenzi mungu kuona kuwa rasilimali hizi zanaanza kupotea zikiwa  mikononi mwetu”,alisema Khamiss Abdallah.

Maonyesho hayo yamejumuisha  nyanja zote za maisha ikiwemo  Mavazi, Ususi, Ufinyanzi, Uhunzi, Uchoraji na Ujenzi  ikiwa ni utaratibu mzima wa mfumo wa maisha ya Wazanzibari.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.