Habari za Punde

Mashindano ya Tahfidh Qur'aan. Msikiti wa Ibadhi Mkoroshoni,Chake Pemba

 Mwanafunzi Amina Azizi Rashid ambaye amehifadhi juzuu 15, akisoma Qur-ani katika mashindano ya Tahfidh Qur-ani yaliyofanyika katika Mskiti wa Ibadhi Mkoroshoni Wilaya ya Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MWANAFUNZI Khamis Ali Mpamba, Mwenye Ulemavu wa Macho (Haoni), akisoma Qur-an katika mashindano ya Tahafidhi Qur-ani, yaliyofanyika huko katika Mskiti wa Ibadhi Mkoroshoni Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MWANAFUNZI Hilali Khamis Ahmed mwenye umri 12, akipokea Charahani baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya Tahfidhi Qur-ani kwa upande wa Juzuu 15, mashindano hayo yaliyofanyika katika Mskiti wa Ibadhi Mkoroshoni Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKUU wa Taaluma katika taasisi ya Samail Academy Pemba, Said Abdalla Nassor akimkabidhi Charahani Mwanafunzi Ummul-kulthum Khamis Jab aliyeibuka mshindi wa kwanza katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an kwa upande wa Juzuu 20, mashindano hayo yaliyofanyika katika Mskiti wa Ibadhi Mkoroshoni Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MWANAFUNZI Mariyam Salum Mohamed mwenye umri miaka 20, akipokea Komputa baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya kuhifadhi Qur-an kwa upande wa Juzuu 30, mashindano hayo yaliyofanyika katika Mskiti wa Ibadhi Mkoroshoni Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 MWANAFUNZI Is-haka Issa Kassim mwenye umri miaka 18, akipokea charahani baada ya kuibuka mshindi wa pili, katika mashindano ya kuhifadhi Qur-an kwa upande wa Juzuu 30, mashindano hayo yaliyofanyika katika Mskiti wa Ibadhi Mkoaroshonio Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MWANAFUNZI Is-haka Bakari Ali mwenye umri wa miaka 10, akipokea baskeli baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya Tahfidhi Qur-an kwa upande wa Juzuu 10, mashindano hayo yalifanyika katika mskiti wa Ibadhi Mkoaroshoni Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MWANAFUNZI Sharif Ali Omar mwenye umri wa miaka 15, akipokea Komputa baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya Tahfidhi Qur-an kwa upande wa juzuu 25, mashindano hayo yaliyofanyika katika mskiti wa Ibadhi Mkoaroshoni Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.