Habari za Punde

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Wapata Elimu ya Maradhi Yasioambukiza

Mratibi wa Jumuiya ya Maradhi Yasioambukiza Zanzibar
(ZNCDA) Bi Zuhura Saleh Ameir akitowa maelezo ya Jumuiya hiyo kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipofika kutowa Elimu ya Maradhi hayo kwa Wajumbe, semina hiyo imefanyika katika Ukumbi mdogo wa Baraza Chukwani Zanzibar.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Mada zinazowakilishwa na Wahusika wakati wa Semina hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Maradhi Yasioambukiza Wizara ya Afya Zanzibar Ndg. Omar Mwalim akitowa mada kuhusiana na lishe wakati wa Semina hiyo kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Wajumbe wakiwa makini kusikiliza Mada hiyo. wakati ikiwasilishwa.

 Mhe Spika wa Baraza la Wawakilishi akizungumza wakati wa Semina hiyo akifafanua jambo kwa wajumbe.  
 Dk Marijani akitowa majibu yaliotolewa wakati wa michango kutoka kwa Wajumbe wa Baraza wakati wa Semina hiyo ya siku moja kutowa Elimu ya Maradhi Yasioambukiza Zanzibar. 
Katibu wa Jumuiya ya (ZNCDA) Ndg. Louis H.Majaliwa akitowa shukrani kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa Michango yao wakati wa semina hiyo iliofanyika katika Ukumbi Mdogo wa Baraza Chukwani Zanzibar. 
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Maradhi Yasioambukiza Zanzibar (ZNCDA) baada ya kumalizika kwa semina hiyo ya kupata Elimu ya maradhi hayo iliotolewa kwa Wajumbe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.