Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa M/Magharibi akanusha uvumi wa kuchinjwa na kuuzwa kwa wanyama waliokamatwa

Na Miza Othman/Khadija Khamis -  Maelezo

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi  Ayoub Mohammed Mahamoud amekanusha  uvumi  wa  baadhi ya wananchi  kuwa  wanyama walioshindwa kugombolewa ndani ya muda uliowekwa, kuchinjwa na kuuzwa  kwa beinafuu Maisara.

Mkuu huyo alisema taarifa hizo hazina ukweli ukweli ni kwamba wanyama hao wataendelea kutunzwa na Serikali kwa kipindi kinachokubalika na kwa wale ambao watakaoshindwa kuwakombowa wanyama wao watataifishwa na kuwa  mali ya Serikali.

Ameyaeleza hayo wakati alipokuwa akizungumza na  waandishi wa habari huko Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibari wakati akitowa taarifa maalumu kwa wananchi wa Mkoa Mjini Magharibi kuhusu Uthibiti wa wanyama kwenye maeneo yasio ruhusiwa.

Hata hivyo  amewataka wafugaji kutokubali kutowa fedha kwa  wahusika na ukamataji wa wanyama  bila ya kupitia taasisi husika (Manispaa), kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa Masheha, Polisi au Manisipaa iwapo kutajitokeza  hali hio ili kuzuia vitendo vya rushwa.

Aidha ameeleza katika utekelezaji wa zoezihilo kumejitokeza  changamoto zikiwemo malalamiko kwa baadhi ya waumini wa dini ambao wanyama wao wanawatumia kwa ajili ya shughuli za ibada wamekamatwa.

Vilevile kumejitokeza kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaohusisha zoezi  hilo na mambo ya kisiasa kwa kuwashajiisha wananchi kuvunja sheria kwa kupingana na utekelezaji wa zoezi hilo.


Alisisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu na  Serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi haitokuwa na muhali katika utekelezaji wa kazi zao  na atakaekwenda kinyume na agizo hilo hatuwa za kisheria zitachukuliwa zidi yake.

Alifahamisha  Utekelezaji wa sheria hizo umekuja kutokana na kukithiri kwa uvunjifu wa nidhamu kwa baadhi ya wafugaji katika maeneo mengi ya  Mkoa wa Mjini Magharibi  jambao ambalo linasababisha uchafunzi wa mazingira, ongezeko la ajali, kukuthiri kwa wizi, kuanza kwa migogoro baina ya wafugaji na wakulima, uharibifu wa miiundombinu pamoja na uhalifu wa kutumia mapanga.

Mahamoud aliwataja wanyama wasioruhusiwa kufugwa ni  Ng’ombe, Punda, Mbuzi na Kondoo na  maeneo yaliyopigwa  marufuku  ni shehia zote za Wilaya ya Mjini , baadhi ya shehia za Wilaya ya Magharibi “B” ambazo Mbweni, Kiiembesmaki, Michungani, Mombasa, Kwamchina, Tomondo, Uzi, Sokoni meli, Melinne, Taveta Mwanakwerekwe, Mikarafuuni, Pangawe Mnarani, Majogoo na Magogoni.

Katika utekelezaji wa zoezi hilo alisema hadi sasa wamefanikiwa kuwakamata jumla ya wanyama 114 kati ya hao Ng’ombe 72, Punda 14  na Mbuzi 28.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.