Na salmin Juma –Pemba
Wafanyabiashara wa soko la Chakechake
mkoa wa kusini Pemba wamedai
kustaajabishwa na mageuzi ya ghafla yaliyofanywa na baraza la mji wa
Chakechake kwa kuwapandishia bei ya gharama za ulipaji kodi kwa 100% pamoja na
upunguzaji wa vikuta vya biashara.
Wakizungumza na mwandishi wa habari
hizi kwa nyakati tofauti baadhi ya wafanyabiashara wa maeneo hayo
wameelezea masikitiko yao kwa kusema kua, hali ya maisha kipindi hiki
ni ngumu mno kwa wakaazi wa kisiwani
humo na wanavyofanyiwa na baraza la mji
kwa kupandishiwa kodi kwa kiwango cha
juu ni sawa na kuwakomoa .
Mmoja miongoni mwa wafanyabiashara
sokoni hapo bw: Rashid Ali Zaina amesema kua uwamuzi uliyochukuliwa na baraza
la manispaa la mji huo ni jambo la ajabu
kwao akisema kua awali waliendesha biashara zao katika mazingira yaliokua
afadhali wakati kikuta kimoja walikilipia Tsh 20,000/= kwa mwezi lakini sasa wametakiwa kukilipia Tsh 50,000/=
hali aliyodai kua inawapa ugumu na kuwaumiza ukilinganisha na mwenendo wa biashara zenyewe
sokoni hapo.
Amesema awali kikuta kimoja alichokua
nacho sasa kimekatwa na kua vikuta viwili na kila kimoja kinatakiwa kulipiwa
gharama hiyo huku akisema kua icho kimoja hakitoshelezi kuwekea bidhaa zao
kutokana na udogo wake.
“kwakweli hali ni ngumu kwasababu hii sehemu
niliyoachiwa hata kama nauza samaki haitoshelezi wakati nna biashara karibu
kumi au kuminatano zote zinataka kupangwa katika eneo hili, sasa utakuta nipo
katika hali ngumu sitaweza hata kufanya lolote katika eneo hili na wanafanya
hivi kwakutukomoa kisiasa na kwakweli uwongozi huu wa baraza la mji wote
hautufai kwa sababu ni watu waliyopandikizwa kisiasa kutukomoa sisi
wapemba”alisema Zaina.
Katibu wa soko bw: Ali Muhammed
Salim amesema kukatwa kwa vikuta hivyo ni uwonevu wanaotendewa na ni
jambo linalo muuma sana kuliko hata wafanyabiashara wengine.
Amesema sokoni hapo wanauowongizi wao
wafanyabiashara lakini wanauwona hauna nafasi
katika jambo lolote kwa baraza la mji
kwa sababu hakuna wanalotatuliwa katika wanayoyasema kama changamoto
kwao.
“Uwongizi wetu hauna nafasi yoyote
kwa baraza hili kwa sababu kama tuna nafasi madai yetu yangekua yanasikilizwa
ingawa tunaitwa na tunawaelezea lakini hayatekelezwi na si hili tu kuna mengi
tushayaongelea, kuna tatizo la vyoo, kama unavyosikia ndugu mwandishi maradhi ya mripuko yaliyomo visiwani mwetu,
tuliomba kurekebishiwa tatizo hilo lakini hatukutekelezewa, tunaukosefu wa maji
lakini hakuna kilichofanyika mpaka leo”alisema Katibu huyo.
Nae mfanyabiashara wa mazao ya
mbogamboga sokoni hapo ambae hakupenda jina lake liandikwe amemwambia mwandishi
wa habari hii kua kodi iliyozidishwa inawapa wakati mgumu kukabiliana na ukali
wa maisha akisema haiwezekani kodi kupandishwa kutoka Tsh 20,000/= mpaka Tsh 50,000/= ukizingatia mkataba haukusema
hivyo.
Amesema hakuna mfanyabiashara
anaepinga kulipia kiasi hicho lakini sikuzote mambo huwenda kwa maafikiano
baina ya wahusika wa pande mbili tofauti na ilivyofanywa na baraza hilo
kuwapadishia kodi kinyume na mkataba waliofungiana.
Akizungumzia suala la ukatwaji wa
vikuta sokoni hapo ameungana na
wafanyabiashara wengine kwa kusema kua , ukubwa wa vikuta walivyokua
wakivimiliki mwazo sasa vimepunguzwa hali ambayo amesema inawapashida pakuziweka
bidhaa zao.
(salminjsalmin@gmail.com)
No comments:
Post a Comment