Habari za Punde

Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Jaji Mshibe Ali Bakar Asema Kesi Nyingi Zinazofunguliwa Zanzibar Hazina Mashiko.

Na Masanja Mabula –Pemba
MWENYEKITI wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Jaji Mshibe Ali Bakar amesema kuwa kesi nyingi zinazofunguliwa katika mahakama za Zanzibar hazina mashiko na zilipaswa kusuluhishwa na jamii kabla ya hazijafikishwa mahakamani .

Amesema kwamba hali hiyo inasababisha kuwepo na mrundikano wa kesi  katika mahakama , kutokana na jamii kuina mahakama kama  sehemu ya kuwasilisha malalamiko hata yale yasiyo na mashiko .

Jaji Mshibe ameyabainisha hayo wakati akifungua kikao cha siku moja cha kukusanya maoni juu ya sheria ya mirathi kwa viongozi wa dini , mahakimu , walemavu pamoja na viongozi wa kisiasa Kisiwani Pemba  katika ukumbi wa Benjemini Mkapa Wete .

Amefahamsha pamoja na kuwepo kwa vyombo vya ulinziz na viongozi wa serikali za mitaa (masheha) lakini wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kuzuia matendo maovu yasitokea ndani ya jamii kabla ya kuwafikisha mahakamani .

“Kwa kipindi kimekuwako na ongezeko kubwa na kesi katika mahakama za Zanzibar na ikizifuatilia utabaini kwamba hazina mashiko , ambazo zilipaswa kusuluhishwa kabla hazijafikishwa mahakamani ”alieleza.

Aidha Mshibe alizidi kufahamisha kwamba kitendo cha jamii kusuluhisha kesi badala ya kufikishwa mahakamani pia kutaokoa fedha nyingi ambazo zilikuwa zitumike kwa ajili ya kuandaa shauri hilo  .

Alieleza kwamba iwapo kila mmoja atawajibika kuzuia matukio yasitokee ndani ya jamii , kutaleta ufanisi wa utendaji wa kazi  serikalini kwani watumishi wake hususani wa mahakama watapunguziwa mzigo wa kupokea mashauri mengi kupita uwezo wa wa kufanya kazi .

“Kama kila mmoja atawajibika kuzuia kesi kufikishwa kutaongeza pia ufanisi wa kazi kwa watendaji wa mahakama zetu , ambao kwa sasa wanapokea kesi nyingi kupita uwezo wa mahakama zenyewe ”alifahamisha.

Hata hivyo akizungumzia suala la kuongezwa watendaji wa Idara ya Mahakama , Jaji Mshibe alisema suwala hilo tayari limepatiwa ufumbuzi , lakini bado changamoto ni jamii yenyewe kutokuwa tayari kufanya suluhu kwa kesi za kawaida .

Akichangia kwenye kikao hicho , Padri wa kanisa la Anglikana Pemba Massoud Emmanuel alisema kwamba , bado jamii haijawa tayari kupokea ushauri na maelekezo kutoka kwa wananchi wa kawaida hata kama utakuwa na maana au faida kwao .

Amesema kwamba viongozi wa dini wanapowajibika katika kuelimisha jamii , hushushiwa zigo wakidaiwa kwamba wamekuwa wanasiasa , jambao ambalo linawawia vigumu kuufikisha ujumbe kwa jamii inayaowzunguka .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.