Habari za Punde

Dk Shein Aendelea kufanya uteuzi


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amefuta uteuzi wa Naibu Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Hafidh Ussi Haji.


Nafasi yake imechukuliwa na Khadija Shamte Mzee, ambae uteuzi wake umefanywa chini ya uwezo aliopewa Rais na kifungu cha 15(1) (A) cha sheria ya Bodi ya Mapato ya mwaka 1996 kama ilivyorekebishwa na kifungu cha 11 cha sheria namba 2 ya mwaka 2000.

Aidha Dk. Shein, amemteua Amour Hamil Bakari kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar kuchukua nafasi ya Abdi Khamis Faki ambaye anastaafu kwa mujibu wa sheria.
Uteuzi wake umeanza Agosti 1,2016 huku uteuzi wa Naibu Kamishna ukianza Julai 25, 2016.

Dk. Shein pia amemteua Umi Aley kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Magazeti ya Serikali, uteuzi ambao ameufanya chini ya kifungu cha 11(a) cha sheria namba 11 ya 2008 iliyounda Shirika hilo.

Said Bakar Jecha na Septuu Mohammed Nassor wameteuliwa kuwa Makamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakati Ali Saleh Mwinyikai ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Zanzibar.

Wengine walioteuliwa ni Maryam Hamdan kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni wakati Maryam Abdulla Yussuf ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani Zanzibar na Prof. Ali Seif Mshimba, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Zanzibar.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza Julai 25, 2016.

1 comment:

  1. Walequm Msalaam, Ahsante kwa kazi zako kutuhabarisha matukio yanayotokea huko nyumbani yawe ya Kisiasa, Kiuchumi, kijamii, Kimazingira na Kiutamaduni. Allah Akupe nguvu na akuimarishie siha yako ili uendelee kutuhabarisha. Ni mimi mdau wa blog yenu kutoka Mji wa Coventry. UK

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.