Habari za Punde

Harakati za Maandalizi ya Sikukuu Mitaa ya Zanzibar leo Mchana.

 Askari wa Usalama barabarani wakiongoza magari katika barabara ya darajani Unguja kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo kipindi hichi cha karibu na Sikukuu Wananchi wengi hufika katika marikiti kuu ya darajani kufuata mahitaji ya maandalizi ya Sikukuu baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Wafanyabiashara ya tungule akiwa na wateja wake kilo moja ya tungule inauzwa shilingi 2000/= kwa kili moja.
Wafanyabiashara ya mbatata na vitunguu wakiwahudumiwa wateja wao katika eneo la darajani Unguja leo ikiwa ni siku ya mwisho ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kilo moja ya mbatata inauzwa shilingi 1000/= na Vitunguu maji kilo moja inauzwa shilingi 1800/=


 Hivi ndivyo ilivyokuwa mandhari ya mtaa wa Darajani ikiwa na Wananchi wengi wakikamilisha mahitaji yao kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Eid Fitr hapo kesho baada ya kuandama kwa mwezi leo na kesho kushrehekea sikukuu hiyo.
Wananchi wa Zanzibar wakiwa katika harakati za hapa na pale kutafuta mahitaji yao kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Eid Fitr inayotarajiwa kufanyika kesho katika viwanja mbalimbali Zanji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.