Habari za Punde

Kisiwani Pemba Azaliwa Ndama wa Ngombe wa Ajabu Anayetowa Harufu ya Mafuta Mazuri.

Na.Salmin Juma- Pemba. 

Katika hali isiyokuwa ya kawaida na ya kushangaza mno leo hii amegundulika ndama wa ajabu anayetoa harufu ya mafuta mazuri puani mwake  wakati akipumua, huko katika kijiji cha kiwapwa Ziwani mkoa wa kusini Pemba.

Ndama huyo anayemilikiwa na bw;Mussa Mohammed Khamis (Borti) mwenye umri wa miezi mitatu amesadifu kuwa na hali hiyo ya kushangaza tangu alipozaliwa na kugundulikana na mchungaji wake hivi karibuni.

Bw; Borti amesema mwanzoni hakuwa ameelewa kuwa harufu ya mafuta mazuri aliyokuwa akiisikia kwamba inatoka puani mwa ng’ombe wake hadi hivi karibuni alipokuwa anamshikilia ili aweze kunyonya kwa mama yake ndipo alipogundua wakati ndama huyo  alipojaribu kutaka kumramba bwana huyo.


Harufu hiyo ya misk pia iliweza kuthibitishwa na naibu sheha wa shehia ya Ziwani bw;Mkubwa Saidi Mkubwa ambaye alihudhuria katika tukio la kuwathibitishia wanahabari juu ya ukweli wa tukio hilo.
Bw; Mkubwa amesema hajawahi hata mara moja kushuhudia tukio la kushangaza kama hilo katika maisha yake licha ya kukaa na kuishi na wanyama kama hao karibu na nyumbani kwake.

Amesema hilo ni tukio la kwanza na la aina yake na kuiomba serekali kupitia kwa wataalamu mbalimbali kufika na kumfanyia uchunguzi ng’ombe huyo ili kujua nini kinachoendelea juu ya tukio hilo.

Aidha bw; Mussa Sharifu amesema yeye ameweza kusikia harufu kali ya spirit inatoka kwa ndama huyo harufu ambayo hatimae ndio hugeuka na kunukia harufu kali ya mafuta mazuri.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.