Habari za Punde

Kuelekea Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Mjini Dodoma, Wajumbe kutoka Mkoa wa Mwanza Waeleza Imani Yao.

Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Simon Mangelepa, akizungumzia maandalizi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho kutoka mkoani Mwanza, ambao tayari wameanza kuwasili mkoani Dodoma kwa ajili ya Mkutano huo ambao unatarajiwa kufanyika Jumamosi Julai 23,2016 ambapo pamoja na mambo mengine pia Mkutano huo ni maalumu kwa ajili ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Katika Mkutano huo, Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM wanatarajiwa kumpitisha kwa kura za ndiyo Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, akipokea Uongozi kutoka kwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka mkoani Mwanza, wamesema wana imani kubwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli ambaye anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa Chama hicho ngazi ya Taifa.

Katibu Mwenezi wa CCM mkoani Mwanza, Simon Mangelepa, ameyasema hayo hii leo, wakati akizungumzia maandalizi ya wajumbe hao ambao baadhi yao tayari wamewasili mkoani Dodoma kwa ajili ya Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaotarajiwa kufanyika Jumamosi ya Julai 23 mwaka huu.

“Sisi wajumbe tunaotoka Mkoa wa Mwanza tunaamini kwamba anatosha (JPM) na yuko makini na chama chetu kitaendelea kuimarika zaidi akikabidhiwa uongozi. Amesema Mangelepa na kuwasihi viongozi wengine wa CCM kuanzia ngazi ya Mashina, Matawi, Kata, Wilaya na Mkoa, kuendelea kukiimarisha chama, ikiwemo kusimamia vizuri Ilani ya uchaguzi katika kuwaletea maendeleo wananchi hususani wanyonge kama Rais Magufuli anavyosisitiza.

Ametanabaisha kwamba wananchi wakiwemo wanaccm, wanayo matumaini makubwa kwa Rais Magufuli katika utendaji wake wa kazi, na kwamba wapenda amani na maendeleo wanaochukia rushwa pamoja na ubadhirifu wanampenda sana.

Katika hatua nyingine Mangelepa amepuuzilia mbali madai yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wanaobeza utendaji kazi wa Rais Magufuli na kwamba hiyo inaashiria hofu waliyo nayo baada ya kukabidhiwa uongozi wa CCM kwa kuwa watakosa hoja za kuzungumza kisiasa.
Bonyeza HAPA Kusikiliza. Au Bonyeza Play Hapo Chini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.